Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA KAMPENI YA CHANJO YA UGONJWA WA SURUA NA POLIO KWA WATOTO, KITAIFA JIJINI ARUSHA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpa tone la dawa ya Chanjo mtoto, Renatha Faustine (1) wakati wa alipokuwa akizindua Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo. Aliyembeba mtoto ni mama wa mtoto huyo, Selina Hando Mkazi wa Moshono Arusha. Kulia ni Agness Joseph mkazi wa Mbulu, akiwa na mtoto wake, Marry Emmanuel, wakisubiri kupata chanjo hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio kwa watoto kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano, Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo.

 Askari wa bendi ya Polisi 'Brass Band' wakiongoza maandamano hayo kupita mbele ya mgeni rasmi.

Wanafunzi wakipita mbele ya mgeni rasmi wakitoa heshima kwa kupiga saluti.


 Vijana wa kikundi cha kwaya cha JKT wakitoa burudani ya kwaya mbele ya jukwaa kuu.
 Vijana wa JKT wakionyesha umahiri wao wa kucheza ngoma ya Kibati.
 Maandamano yakipita mbele ya Jukwaa Kuu.
 Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo wa Chanjo.
 Maandamano ya wanafunzi wakipita mbele ya Jukwaa Kuu.
Watoto wa Shule za Msingi, wakipita mblele ya jukwaa la mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya  Chanjo ya ugonjwa wa Surua na Polio.
Maandamano...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.