Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi, lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akimpa maelezo kuhusu kinywaji cha kienyeji Pombe ya Chimpumu inayotumiwa na Kabila la watu wa Rukwa, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowasilishwa na na Kabila la Jamii za Mikoa ya Rukwa na Katavi, lililofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimshuhudia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda , akinywa kinywa cha asili aina ya Chimpumu ‘Pombe ya Isute’ kinachotengenezwa na Kabila la watu wa Katavi na Rukwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka ndani ya nyumba ya asili ya watu wa Kabila la Wafipa, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akimpa maelezo ya jinsi ya kutengeneza Jembe la Asili la Ufipa linalotengenezwa kwa kutumia Chuma cha asili kinachofuliwa na watu wa Rukwa na Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Manyanya (kuli) akishiriki kucheza ngoma ya asili ya kabila la watu wa Rukwa wakati wa Tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment