Habari za Punde

*MAMA ZAKHIA BILAL AZINDUA KUNDI NA ALBAM YA KWANZA YA T-MOTO 'REAL MADRID'

  Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akivuta utepe kuzindua rasmi kundi jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ‘Real Madrid’ wakati wa uzinduzi wa kundi hilo na albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku. Kushoto ni Mkurugenzi wa kundi hilo, Amin Salmin.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akipokea zawadi ya Cd za kundi la T-Moto, kutoka kwa Mkurugenzi wa kundi hilo, Amin Salmin, baada ya Mama Zakhia kuzindua rasmi kundi hilo jana usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee. Katikati ni Mama Tunu Pinda
  Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ‘Real Madrid’, Amin Salmin, akizungumza jukwaani wakati wa uzinduzi wa kundi hilo, uliofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Mgeni Rasmi Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akizungumza jukwaani baada ya kuzindua rasmi kundi na albam ya kwanza ya kundi jipya la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) uzinduzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana Usiku.
 Waimbaji wa bendi ya Mapacha Wa3 kutoka (kushoto) Kalala Junior, Jose Mara na Khalid Chokoraa, wakishambulia jukwaa wakati walipokuwa wakisindikiza uzinduzi wa Kundi la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku.
 Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Mosi Suleiman, akiimba jukwaani wakati wa uzinduzi wa Kundi na  albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam jana usiku.
 Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Bi Mwanahawa Ally, akiimba jukwaani kibao chake cha Aliyeniumba Hajanikosea, wakati wa uzinduzi wa Kundi na  albam ya kwanza ya kundi hilo.
 Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Jokha Kasim,  akiimba jukwaani kibao chake cha Unavyojidhan Haufanani.
Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Mrisho Rajab, akiimba jukwaani kibao chake cha Mchimba Kaburi Zamu yake Imefika.

Mama Zakhia Bilal, Mama Tundu Pinda, Mama Kawawa, wakiwa katika picha ya pamo wasanii wa kundi la T-Moto baada ya kuzinduliwa rasmi.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.