Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua Serikali.
Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7.
Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha.
Baada ya kutolewa Jela, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke.
Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wakisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlaani na kumtenga.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya Uhuru, Bibi Titi alionekana katika makaratasi ya chama tawala CCM kama"Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Bibi Titi alifariki kwenye hospitali ya 'Net Care Hospital' ya mjini Johannesburg ambako alikuwa akitibiwa.
Moja kati ya barabara kubwa za jijini Dar es Salaam imepewa jina la Bibi Titi kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.
No comments:
Post a Comment