Habari za Punde

*STARS YAWASILI N'DJAMENA, POULSEN ATAJA KIKOSI CHA KWANZA

Timu ya Taifa 'Taifa Stars' imewasili jana usiku N'Djamena tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa kesho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya.

Timu imefikia hoteli ya Santana, na leo saa 10 jioni kwa saa za hapa itafanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya na mchezo huo unatarajia kupigwa kesho kuanzia  saa 10 kamili jioni ambayo sawa na saa za hapa nyumbani saa 12 jioni.
Wachezaji wote wako katika hali nzuri isipokuwa beki Erasto Nyoni, ambaye ameamka leo asubuhi akiwa na malaria.

Waamuzi wote wanatoka Nigeria. Mwamuzi wa kati atakuwa ni Bunmi Ogunkolade, wakati wasaidizi ni Tunde Abidoye na Abel Baba. Kamishna wa mechi ni Hamid Haddadj kutoka Algeria.
Stars imewasili Ndjamena na kikosi cha wachezaji 21 ambacho kitarejea nyumbani siku moja baada ya mechi kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia. Timu itawasili Novemba 13 mwaka huu saa 7.25 mchana na kwenda moja kwa moja kambini.
Kocha Jan Poulsen ametaja Kikosi cha kwanza kitakachoanza kuikabili Chad kesho kuwa ni pamoja na, Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Juma Nyoso, Idrisa Rajab, Shabani Nditi, Henry Joseph, Abdi Kassim, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa na Mbwana Samata.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.