Habari za Punde

*TAIFA STARS WAREJEA DAR KUJIANDAA KUWAKABILI CHAD KESHOKUTWA

Wachezaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni baada ya kumaliza kazi ya kuaadhibu Chad nyumbani kwao kwa mabao 2-1. Stars imewasili leo na inaingia kambini kujiandaa na mchezo wa marudiano na Chad unaotarajiwa kupigwa Jumanne Novemba 15 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Stars itahitaji sare ya ama ushindi wa aina yeyote ili kuweza kujihakikishia tiketi ya michuano hiyo.
Henry Joseph na Nizar Khalfan, wakitoka nje ya uwanja huo leo.
Kocha Mkuu wa Stars, Jan Poulsen, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Julius Nyerere.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.