Habari za Punde

*TWANGA PEPETA YAZINDUA ALBAM YAKE YA 11 'DUNIA DARAJA'


BENDI ya muziki wa dansi nchini, The African Stars “Twanga Pepeta” International jana iliweka historia mpya katika muziki wa dansi baada ya kuzindua albamu yake ya 11Ijulikanayo kwa jina la Dunia Daraja kwa kujaza umati wa watu mithiri ya tamasha la kila mwaka la Fiesta.
Mbali ya umati wa watu katika uwanja wa mchezo wa kriketi, bendi hiyo pia iliibuka na kituko kingine baada ya waimbaji wake wakiongozwa na kiongozi wao, Luizer Mbutu wakingia viwanjani hapo wakiwa kwenye gari aina ya Land Rover Breakdown maarufu kwa jina la ‘Fisi’.
Hali hiyo iliwafanya mashabiki hao kushikwa na butwaa na wengine wakifurahia kutokana na kituko hicho. Breakdown hiyo iliyokuwa na namba ya usajili T720 ABL ikuwa kuu kuu na waimbaji hao walikaa mbele ya bodui na wengine wakiwa pembeni.
Baada ya kushuka stejini, wanamuziki bendi hiyo ilipiga moja kwa moja wimbo uliobeba jina la albamu hiyo, Dunia Daraja uliotungwa na Chalz Baba. Wimbo huo unazungumzia sehemu ya historia ya bendi hiyo hasa mitindo yake, kutesa kwa zamu, Kidali Po, Mgongo Mgongo, Kusugua Kisigino na sasa Watu Wazima Ovyo.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa wamefarijika na ujio wa mashabiki ambao wameonyesha kuikubali bendi hiyo na hiyo imehashiria kuwa ukumbi ambao wamezoea kuzindulia, Diamond Jubilee ni mdogo kulingana na soko lao la sasa.
“Huu umati ningeuweka wapi pale (Diamond), tuliamua jambo la maana sana kufanyia hapa (Leaders Club), kwa kweli tumefarijika sana nah ii inaonyesha hadhi halisi ya bendi,” alisema Asha.
Nyimbo nyingine za albamu hiyo ni "Penzi la Shemeji" uliotungwa na Muumin Mwinjuma, "Mtoto wa Mwisho" (Dogo Rama), Kauli, (Luizer Mbutu), na Kiapo Cha Mapenzi wa Saleh Kupaza.

 Wanamuziki wa bendi hiyo, wakipanda jukwaani kwa staili yao mpya wakati wa uzinduzi huo. Picha Zote na Majuto Omary (Mwenyekiti wa TASWA Fc)
 Wanamuziki wa bendi hiyo wakishambulia jukwaa.
Mnenguaji wa bendi hiyo, Lilian Internet, akiwapagawisha mashabiki wake...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.