Habari za Punde

*WANANCHI WA LIBERIA KUPIGA KURA UCHAGUZI WA RAIS LEO HII

Polisi wa kutuliza ghasia mjini Monrovia Polisi wa kutuliza ghasia mjini Monrovia
*Duru ya pili ya uchaguzi wa rais Liberia
Raia wa nchini Liberia leo watapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Katika duru ya uchaguzi wa kwanza wa rais wa sasa, Ellen Johnson Sirleaf, alipata asilimia 44 ya kura zote.
Hata hivyo, mgombea wa Upinzani, Winston Tubman, anasusia duru ya pili akidai kuwa uchaguzi hautakuwa wa huru na haki.
 
Wafuasi wake waliokabiliana na maofisa wa polisi hapo jana wametishia kuvuruga shughuli za upigaji kura wa leo.
Rais Barrack Obama wa Marekani ametoa wito kwa wananchi wa Liberia kuendesha kura huru na za haki na kuonya dhidi ya majaribio ya kuvuruga mchakato huo wa uchaguzi.

Inaaminika mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi katika mkutano wa kampeni ya chama cha upinzani katika mji mkuu Monrovia, hapo jana.

Idadi ndogo ya wapigaji kura itamaanisha kuwa Bibi Ellen Johnson Sirleaf, ambaye hivi majuzi alishinda tuzo ya amani ya Nobel ataongoza nchi iliyogawanyika.

Lakini iwapo raia wa Liberia watajitokeza kwa wingi, basi ataweza kudai ushindi kamili, Imeelezwa.
Wakosoaji wanasema kuwa,Tubman anajiondoa katika kinyanganyiro hicho kwa kuwa anahofia kushindwa na rais wa sasa, Ellen Johnson Sirleaf.

Katika mji mkuu Monrovia, wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa pamoja na askari wa Liberia wamedumisha usalama.

Miaka minane baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo watu zaidi ya 200,000 waliuawa, mapigano mapya huenda yakasababisha Liberia irudi tena katika machafuko.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.