Habari za Punde

*YANGA YAMREJESHA CHUJI KIKOSINI KUKIPIGA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU

MABINGWA Timu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga ya Jijini Dar es Salaam, imeamua kumrejesha kundini aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Athuma Idd 'Chuji' katika usajili wa dirisha dogo.

Timu hiyo ilimtema kiungo huyo katika usajiri uliopita ambapo aliamua kujiunga na timu ya Simba ambako pia alitimka baada ya kuzinguliwa na uongozi wa timu hiyo na kuwa na utata hukua kielezwa kuwa ni mchezaji wa Villa na mara akisomeka katika usajiri wa samba.
Chuji amesajiliwa kwa ajili ya kuitumikia Klabu hiyo katika mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
Habari za kuaminika kutoka Yanga zinasema kwamba Chuji alimwaga wino wa kuichezea timu hiyo kwa miaka miwili baada ya kukamilisha mazungumzo kati yake na Uongozi wa kamati ya usajili.

“Ni kweli tumemsainisha Chuji kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kukamilika kwa mazungumzo, hivyo Chuji ni mmoja kati ya wachezaji watakoavaa uzi wa Njano na Kijani katika mzungo wa pili wa ligi kuu bara na michuano ya kimataifa,”Alisema kiongozi mmoja wa Yanga ambaye hakupenda kutajwa jina lake.

Hata hivyo, huenda klabu hiyo ikaingia tena katika mgogoro wa kumgombea mchezaji huyo na mahasimu wao Simba ambayo mwaka huu ilimsainisha mkataba kabla ya kumpeleka kwa mkopo katika klabu ya Villa Squad.

Kitendo cha kuuzwa kwa mkopo Villa Squad haikumridhisha Chuji ambaye aligoma kuichezea timu hiyo na kudai kuwa yuko radhi kuuza karanga kuliko kwenda kuichezea timu hiyo inayosuasua kwenye ligi hiyo.

Kama hiyo haitoshi, Chuji alitishia kuchukua sheria kwa wekundu wa msimbazi ambapo kupitia kwa mwanasheria wake, alitishia kusimamisha ligi iwapo asingerejeshwa Simba, lakini Simba walibaki na msimamo wao wakutokubali kumtumia kiungo huyo kwa kusema wameshavunja mkataba na Chuji.
Nalo Shirikisho la soka Tanzania (TFF) baada ya msigano huo, liliendelea kusisitiza kuwa Chuji ni mchezaji halali wa  Simba kwa kuwa aliingia nao mkataba wa kuichezea miaka miwili, pia kuwa na leseni na ndio maana akapata nafasi ya kuichezea katika michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’.
Aidha, TFF ilisema kwamba kwa vigezo hivyo anaweza kushitaki kwao kama atajihisi kuonewa baada ya Simba kudai kuwa hawamuhitaji kwenye kikosi chao kitakachoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuanzia Agosti 20.
Habari hii na Mama Pipiro Blog

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.