Habari za Punde

*25 WAITWA TWIGA STARS KUJIANDAA KUIKABILI NAMIBIA

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Wanawake 'Twiga Stars' Esther Chabruma akikabiliana na mabeki wa Elitrea katika moja ya mchezo wa timu hizo.
 
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars), Charles Boniface Mkwasa leo  ametaja kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Namibia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkwasa, alisema kuwa mechi ya kwanza itachezwa jijini Windhoek, Namibia kati ya Januari 14 na 15 mwaka huu, na ile ya marudiano itachezwa Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Aidha alisema kuwa Kikosi hicho kinatarajia kuanza mazoezi Desemba 19 mwaka huu kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ambapo  wachezaji waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti ofisi za TFF siku hiyo saa 9 alasiri tayari kwa kuanza mazoezi.
Aliwataja wachezaji walioitwa kuwa ni Sophia Mwasikili (Sayari Women), Fatuma Bushiri (Simba Queens), Fatuma Omari (Sayari Women), Mwajuma Abdallah (JKT), Asha Rashid (Mburahati Queens), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Ettoe Mlenzi (JKT), Zena Khamis (Mburahati Queens), Fatuma Khatib (Mburahati Queens), Maimuna Said (JKT), Fadhila Hamad (Uzuri Queens), Fatuma Mustapha (Sayari Women) na Evelyn Senkubo (Mburahati Queens).
Rukia Hamisi (Sayari Women), Mwapewa Mtumwa (Evergreen), Judith Hassan (TMK), Aziza Mwadini (Zanzibar), Sabai Yusuf (Zanzibar), Semeni Abeid (Tanzanite Queens), Zena Said (Uzuri Queens), Pulkaria Charaji (Sayari Women), Tatu Said (Makongo Sekondari), Mwanaidi Hamisi (Uzuri Queens), Hanifa Idd (Uzuri Queens) na Fatuma Gotagota (Mburahati Queens).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.