Habari za Punde

*RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA MKUTANO WA KUPINGA UNYANYASAJI NA UKATILI WA KIJINSIA KAMPALA LEO

Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda huku Katibu Mtendaji wa Kamati ya Kimataifa ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) anayemaliza muda wake Balozi Liberata Mulamula akitega sikio katika siku ya pili ya mkutano huo wa viongozi wakuu wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia uliofanyika kwenye hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongoji cha Munyonyo, Kampala, leo.
Rais Jakaya Kikwete akichangia mada katika siku ya pili ya mkutano huo wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongoji cha Munyonyo, Kampala, leo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais Michael Satta wa Zambia na mkewe usiku wa kuamkia leo, muda mchache kabla hawajaelekea Ikulu ya Entebbe ambako, Rais Yoweri Museveni aliandaa chakula cha usiku kwa wajumbe wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.