Habari za Punde

*BENDERA AFUNGUA KONGAMANO LA KWANZA LA WARATIBU WA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera , akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo la Bima ya Afya, la kwanza la Waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) nchini, lililofanyika mjini Morogoro jana. Picha na Richard Mwaikenda
 Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Khamis Mdee, akifafanunua mambo mbalimbali yahusuyo mfuko huo wakati wa kongamano hilo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba (kulia), akiwaeleza waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), umuhimu wa kuuboresha mfuko huo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho, wakati wa kongamano la kwanza la waratibu wa mfuko huo nchini, lililofanyika kwenye Hoteli ya Kisasa ya Nashera, mjini Morogoro, jana.
 Baadhi ya Waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) nchini, wakishiriki katika kongamano la kwanza la kujadili na kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za mfuko huo, lililofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, mjini Morogoro jana.
Moja ya makundi ya Waratibu wa CHF, wakijadiliana jinsi ya kuweka mikakati ya uboreshaji wa mfuko huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.