Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, akikata utepe kuzindua rasmi wa duka jipya la kisasa la kampuni ya Vodacom lilipo katika jengo la Quality Center barabara ya Pugu jijini Dar es salaam litakalotoa huduma kwa wateja pamoja na mauzo ya bidhaa mbalimbali za Vodacom. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Vodacom Kanda ya Pwani, Henry Tzamburakis.Uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki jijini.
***************************************
Na Mwandishi Wetu, Jijini
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua duka jipya la kisasa lililopo katika jengo la kibiashara la Quality Center, kwa ajili ya kuhudumia wateja wake pamoja na kufanya mauzo likilenga kusogeza karibu zaidi huduma kwa wateja wake.
Akizindua duka hilo mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisifu juhudi za Vodacom za kutoa huduma bora kwa wateja huku akiwataka kuongeza ubunifu ili kuwanufaisha watumiaji wa huduma za simu za mkononi nchini.
“Nimefurahi kuwa hapa leo kuzindua duka lenu, nawapongeza kwa juhudi zenu za dhati mnazozifanya katika kutoa huduma bora na namna mnavyowahudumia wateja wenu na uwepo wa duka hili utapanua wigo wa kuwahudumia kwa uharaka, urahisi na ukaribu zaidi”Alisema Rugimbana muda mfupi baada ya kufanya uzinduo huo na kupata fursa ya kutembelea duka hilo lililopo barabara ya pugu jijini Dar es salaam.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema mpangilio wa duka hilo pamoja na mahali lilipo ni wazi litatoa faida kubwa kwa jamii na wateja wa Vodacom kampuni inayoongoza soko la huduma za mawasiliano ya simu za mkononi kwa kuwa na wateja zaidi ya milioni kumi na moja.
“Kadri mnavyosogeza huduma zenu karibu na wateja ndivyo hivyo mnavyoongeza urahisi wa maisha kwa wateja ambao bila ya hivyo watalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata maduka hayo ili waweze kupata huduma ikiwemo kutatuliwa matatizo wanayokabiliana nayo katika kutumia huduma za mawasiliano ya simu”Aliongeza Rugimbana huku akitoa rai kwa wananchi kutumia fursa za maduka hayo kuwa karibu nao kujipatia huduma na kujifunza.
Awali akimpatia maelezo Mkuu wa Wilaya. Meneja Mauzo wa kampuni ya Vodacom Kanda ya Pwani Bw. Henry Tzamburakis alisema kufunguliwa kwa duka hilo kunalenga kutoa urahisi kwa wateja wa Vodacom kupata huduma bora.
Amesema hilo ni duka la kumi na moja katika mkoa wa Dar es salaam mbali na maduka madogo madogo yaliyozagaa kila kona yanaitwa Vodacom Duka ambayo kwa pamoja yanatenegza mtandao mpana wa kuhudumia wateja na jamii kwa ujumla kwa ukaribu zaidi katika kiwango cha ubora wa hali ya juu
“Hili ni duka letu la kumi na moja katika mkoa wa Dar es salaam ni azma ya Vodacom kuona kwamba mteja anahudumiwa na kufikiwa na huduma kwa uharaka na urahisi zaidi ili waweze kujiskia ufaghari kuwa miongoni mwa familia kubwa ya wateja zaidi ya milioni kumi na moja”Alisema Tzamburakis.
Amesema ukuaji wa Vodacom katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi unachagizwa pamoja na mambo mengine na udhati wa kampuni hiyo katika kuwahudumia wateja wake kwa kiwango cha ubora unaoendana na hadhi ya kampuni bila kujali aina ya mteja anaehudumiwa kwa kuzingatia kwamba kila mteja wa Vodacom ana haki sawa ya kupata huduma bora zitakomfanya mwisho wa siku kutabasamu.
“Tumethubutu kuleta duka hili katika eneo hili la biashara tukiamini litawahudumia vema wateja wetu wa maaeneo ya Buguruni,Gongolamboto, Chang’ombe, na maeneo mengine ya Wilaya ya Temeka na Ilala hivyo ni imani yetu kwamba kwa hatua hii wataendelea kujivunia kuwa wateja wa kampuni ya Vodacom”Alisema Tzamburakis
Tzamburakis amesema Amesema duka hilo litatoa huduama zote kwa wateja ikiwemo huduima za M-PESA, usajili, manunuzi ya muda wa hewani na bidhaa mbalimbali za Vodacom ikiwemo WEB BOX simu za mkononi na Moderm na kwamba ni azma ya Vodacom kuimarisha mtandao wa maduka yake nchi nzima ili kuendana na kasi ya ukuaji kibiashara na mahitaji ya wateja sokoni.
No comments:
Post a Comment