Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokutana na Watanzania waishio nchini Burundi jana usiku. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dkt. James Mwasi Nzagi (kulia) ni Mwenyekiti wa Kinamama wa Jumuiya ya Kinamama waishio Burundi, Siwajibu Hamis (wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa Vijana wa Jumuiya hiyo, Mutalemwa Julian.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Watanzania waishio Bujumbura Burundi, baada ya kumaliza mazungumzo baina yao yaliyofanyika jana usiku na kujadili mambo mbalimbali yanaoendelea katika Taifa la Tanzania.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi (katikati) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi J Mahadhi (kulia) Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, wakifurahia jambo kwa pamoja wakati wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura Burundi wakisubiri kuondoka kurejea nchini leo baada ya kuhudhuria Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu uliomalizika nchini humo juzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza, wakati akiwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Burundi leo mchana tayari kwa kuondoka nchini humo kurejea Tanzania baada ya kumaliza shughuli za Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu, uliomalizika Bunjumbura Burundi juzi.
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma ya asili cha Burundi wakionyesha umahiri wao wa kucheza ngoma hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa maalum kwa ajili ya viongozi waliohudhuria Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu Bujumbura Burundi. Hafla hiyo ilifanyika juzi jioni baada ya kufungwa rasmi kwa mkutano huo.
Mtoto akionyesha umahiri wake wa kucheza miondoko ya ngoma hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni.
Askari wakiimalisha ulinzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Bujumbura.
No comments:
Post a Comment