Hawa ni baadhi tu ya Vijana wanaojiwezesha kumudu sehemu kubwa ya maisha yao kutokana na mazoezi wanayofanya kwa ajili ya kujiweka fiti na kuvimbisha miili, ambapo wamekuwa wakijipatia kipato ama ajira kulingana na 'Bodi' zao.
Tumezoea kuwaona vijana hawa wengi wao wakiwa katika mageti ya Kumbi maarufu za starehe kwa lengo la kulinda usalama, lakini siku hizi watu hawa wamekuwa na kazi nyingi kulingana na mteja anavyowapangia.
Tumesikia siku za hivi karibuni Mabaunsa kama hawa wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya watu wenye fedha zao kwa ajili ya kuwahamisha wananchi katika maeneo fulani na wengine wamekuwa wakitumiwa kuvunja ama kubomoa Nyumba za watu wanaokuwa wamegoma kuhama mahala fulani baada ya eneo hilo kuuzwa.
Kwa kweli Vijana kama hawa hivi sasa wamekuwa ni Tegemeo kila kona kama ambavyo walikutwa Vijana hawa wakijiandaa kwa ajili ya kubeba Kijikiti kidogo tu kilichokuwa na Kijitabu kidogo juu yake na kuingiza ukumbini wakati wa Hafla ya kukabidhi Tuzo za Super Brands kwa Makampuni yaliyofanya vizuri mwaka 2011, iliyofanyika jana usiku katika Ukubi wa Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky. Hongereni Vijana kwa kujiajiri kupitia miili yenu Wenyewe.
Kijana akionyesha misuri yake wakati akipasha kabla ya kuanza kazi yake hiyo.
Vijana hawa akipasha kuweka misuri sawa kabla ya kuanza kazi yao.
No comments:
Post a Comment