Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (kushoto) na Ofisa wa Mfuko wa Kusaidia Jamii wa kampuni hiyo, Grace Lyon, wakishusha viloba vya mchele, unga wa sembe,sukari na maharage vilivyotolewa na Vodacom kusaidia kambi ya waathirika wa mafuriko ya Dar es salaam ya Hananasifu juzi. Wa kwanza kulia ni Mfanyakazi wa Vodacom, Lilian Kisamba, akisadiana na wasimamizi wa kambi hiyo kupokea vyakula hivyo.
Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, (kulia) akimtiwsha Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mkunguni B, kata ya Hananasifu, Andrew Mkude kiloba cha sukari. Vodacom ilikabidhi mchele, sukari, unga wa sembe, mikate na maji ya kunywa kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam wanaojihifadhi katika kambi ya Hananasifu juzi.
Ofisa wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, akisaidiana na mmoja wa wasimamizi wa kambi ya waathirika wa maafa ya Dar es salaam kambi ya Green Acre Magomeni kubeba kiloba cha mchele tayari kukabidhiwa kwa waathirika.
No comments:
Post a Comment