Habari za Punde

*WAKALI KALAMA NYILAWILA NA FRANSIC CHEKA USO KWA USO JANUAR 28

Francis Cheka akiwa katika mazoezi ya kujiandaa na pambano hilo.
MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka (SMG) na bingwa wa Dunia, Karama Nyilawila (Kapten) wanatarajia kupanda ulingoni Januari 28 mwaka huu kuoneshana umwamba.
Mabondia hawa kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta fulsa ya kupambana huku kila mmoja akimtambia mwenzake kulingana na ubingwa wake ambapo hawajawahi kuandaliwa pambano la kuwakutanisha, jambo ambalo liliwafanya mashabiki masumbwi kuhisi kuwa mabondia hao wanaogopana.

Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto, jijini Dar es Salaam jana, Promota wa pambano hilo Philemon Kyando 'Don King' alisema pambano hilo la raundi 10 la uzito wa Kg 72, litapigwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro nyumbani kwa Cheka.
Aidha Kyando, alisema kuwa, pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kati ya Maneno Osward (Mtambo wa Gongo) atakayezichapa na Pasco Ndomba, pambano la raundi nane uzito  wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku kg 68, Venance Mpoji na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert Mbena kg 54 ambapo mapambano yote  yatakuwa ya raundi sita kila moja.

“Tumeamua  kuandaa pambano hili la Nyilawila na Cheka, ili kuondoa ubishi na utata baina yao na maneno ya mashabiki wenye hamu ya kuona watu hawa wakipanda ulingoni, kwani hawajawahi kushuhudia pambano la wakali hawa wakikutana” alisema Promota


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.