SERIKALI ya wilaya ya Manispaa ya Iringa imepiga marufuku walimu wakuu wa shule ya sekondari wilayani Iringa kuendelea kuchangisha wazazi fedha za michango ya madawati wakati madawati yakiendelea kukaa bila kutumika katika shule hizo.
Hatua ya serikali kupiga marufuku michango hiyo ya madawati imekuja baada ya wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo kuhoji sababu ya walimu kuendelea kuagiza madawati wanafunzi kila mwaka huku wanapomaliza kidato cha nne hawaondoki na madawati hayo.
Kutokana na malalamiko hayo mkuu wa wilaya ya Iringa Aser Msangi (pichani) alitaka walimu wa shule hizo za sekondari ambazo ndizo zinaongoza kwa michango ya madawati kujaribu kubuni mradi mwingine wa kupata fedha badala ya kuendelea kuchangisha wazazi fedha za madawati kila mwaka wakati madawati mengine yakiendelea kukaa stoo bila kutumika.
"Nawashauri walimu kama madawati yapo wasiendelee kuwachangisha wazazi madawati badala yake watafute miradi mingine wananchi kuchangia isiwe madawati pekee kwani itafika sehemu wananchi watachoka". DC
Hata hivyo alisema kuwa hapigi marufuku michango mbali mbali kwa ajili ya maendeleo ya shule ila anapingana na utaratibu wa wakuu hao wa shule kila mwaka kuchangisha madawati na kuwa miradi ipo mingi hivyo wananchi kuchangishwa fedha isiwe madawati pekee.
SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU NCHINI
-
Na Mwandishi wetu -Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) imeendelea ...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment