*Ubalozi na Watanzania wafanya kweli Ujerumani !
*Ngoma Africa Band aka FFU ! wamedatisha waheshimiwa na wadau wote ! Berlin,
Siku ya Ijumaa ya 9.12.2011 na jumamosi 10.12.2011 Watanzania waishio Ujerumani na nchi jirani wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani,walilitingisha jiji la Berlin kwa masaa kadhaa wakati walipokuwa wakisherehekea sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara.
Sherehe hizo zilizoongozwa na Balozi Bw.Ngemela na maofisa wa ubalozi akiwemo Bw.Ali Siwa, zilianzia katika ukumbi wa Martim ambako kulikuwa na mkusanyiko wa mabalozi wa nchi mbali mbali,vingozi wa ngazi za juu wa serikali ya Ujerumani,watanzania, mashirika NGO's,na marafiki wahisani wa Tanzania walikuwapo kusherekea na kuipongeza Tanzania kwa kufikia miaka 50 ya uhuru kwa amani.
Tanzania pia ilipongezwa na kutajwa kuwa nchi ya Amani barani afrika ambayo wananchi wake wameshikama kwa amani na upendo.
Ngoma Africa Band aka FFU chini ya uongozi wake Ras makunja aka Kamanda wa FFU, muziki wa bendi hiyo ulifanaikiwa kuwachanganya uwanjani madipromasia na wadau walioudhuria katika sherehe hizo ijumaa na jumamosi bendi hiyo maarufu inatamba na CD mpya Shangwe 50 Uhuru anniversary.
Pia sherehe hizo ziliambata na ufunguzi wa chama cha Watanzania ujerumani (UTU) ambacho kilifunguliwa rasmi siku ya jumamosi 10.12.2011 na Balozi Mhe.Ngemera ambaye pia ndie aliyetilia mkazo kwa kuanzishwa kwa umoja huo ambao ndio mwamvuli wa watanzania wote waishio Ujerumani,Umoja huo umesajaliwa na serikali ya Ujerumani kama NGO's na mwenyekitiki wake Bw.Mfundo Peter Mfundo.

Ngoma Africa Band aka FFU, wakishambulia jukwaa.
No comments:
Post a Comment