Habari za Punde

*BARABARA YA KILWA KUANZA KUJENGWA UPYA-MAGUFULI

Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli,  akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara ya Kilwa utakaofanyika sambamba na upanuzi wa barabara hiyo yenye jumla ya  Kilomita 5.1 kwa kiwanga cha lami itakayojengwa na mkandarasi wa Kajima Corporation. Kulia ni Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mh. Masaki Okada.
Alisema kuwa Serikali imefikia maafikiano na kampuni hiyo na kuamua kufanya ujenzi wa Barabara hiyo  kurudiwa kujengwa kwa mara ya pili baada ya kampuni hiyo kuifanya kazi hiyo chini ya kiwango na boronga katika ujenzi wa awali.
Aidha Waziri Magufuli ameongeza kwamba Mkandarasi ataondoa tabaka la lami katika urefu wa Kilomita 5.1 na tabaka jipya la lami lenye unene wa sentimeta 7 akitumia lami yenye kiwango cha ugumu cha 40/50 na kokoto za ukubwa wa milimita 20,  ‘zege la lami (Asphalt Concrete)’  lenye kokoto za ukubwa wa milimita 20 (AC 20), lami iliyoimarishwa zaidi itafikiriwa kutumika sehemu za barabara zenye kubeba mzigo mkubwa zaidi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.