Na Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya Kijitonyama Veterans leo (kesho Jan 5) inacheza mchezo maalumwa kirafiki dhidi ya timu ya Chuo cha Usafirishaji cta Taifa (NIT).
Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 10.00 jioni kwenye uwanja wa Chuo Cha Usafirishaji kwa mujibu wa Mratibu na kocha mkuu wa Kijitonyama Veterans, Majuto Omary.
Majuto alisema mchezo huo umeandaliwa kwa ajili ya kujenga mahusiano baina ya NIT na timu yao ambayo imekuwa na matokeo mazuri sana katika mchezo wa soka. Mkuu wa chuo hicho, Zakaria Mganilwa atakuwa mgeni rasmi katika mchezo huo.
Alisema kuwa wachezaji wa Kijitonyama Veterans wana morali ya hali ya juu na hasa baada ya kufanya vyema katika mechi mbali mbali mwaka jana.
“Mpaka sasa timu yetu imeweka historia kubwa baada ya kutwaa ubingwa wa bonanza la miaka 50 ya Uhuru iliyofanyika Desemba 9 mwaka jana, hii ni mechi yetu ya kwanza mwaka huu na tumeadhimia kuweka historia kwa kuanza vyema mwaka 2012,” alisema Majuto.
Aliwataja wachezaji nyota wa timu hiyo kama Said Seif, Isihaq “Niyonzima” Said, Kiki de Kiki “Tom Mawejje”, Hamis Kayuga na wengine wengi wataiongoza jahazi la timu yake leo.
Msemaji wa timu ya NIT, Leonard Sempoli alisema kuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo huo na baada ya mechi hiyo, wameandaa shereh rasmi ya ukaribisho.
“Tunatarajia kuwa na mechi nzuri nay a aina yake, lengo kuu ni kufahamiana na tunatarajia kucheza mechi nyingi na timu nyingine,” alisema Sempoli.
No comments:
Post a Comment