Habari za Punde

*MFANYAKAZI WA NDANI YATIMA, AZALISHWA NA SHAMBA BOY NA KUTELEKEZWA AHAHA NA MWANAE KUSAKA MSAADA

Mtoto yatima Hawa Saidi (19) mkazi wa kijiji cha Ulembo wilaya ya Njombe mkoani Iringa amejikuta akiishi tena katika mazingira magumu na mwanae kwa kuhangaika mitaani na mtoto wake huyo wa mwaka mmoja, baada ya kuzalishwa na mfanyakazi mwenzake wa kazi za ndani na kufukuzwa kazi.
 
Binti huyo ambaye jana usiku alikutwa akizunguka katika mitaa ya Frelimo muungano katika Manispaa ya Iringa, anadai kuwa wazazi wake walifariki tangu akiwa darasa la kwanza na kulazimika kukatisha masomo yake na kwenda Dar es Salaam kusaka kazi kwa kipindi cha miaka miwili kwa mshahara wa shilingi 20,000 kwa kila mwezi.

Alisema kuwa kwa sasa hana njia nyingine ya kuishi na hivyo kuomba wasamaria wema kumsaidia kurudi shule ama kupewa kazi ya ndani ili kuweza kusomesha mtoto wake na yeye mwenyewe kupata uhakika wa maisha.

Hivyo kama upo tarayi kumsaidia waweza kuwasiliana na mwandishi wa Iringa Francis Godwin, kupitia namba 0754 026299/0712750199 ili kuweza kumsaidia kwa lolote binti huyo.


1 comment:

  1. Pole sana binti lakini usikate tamaa Mungu yupo pamoja na watu wote kwa hiyo hawezi kukutupa.Jitahidi kusimamisha IBADA (kuswari) Wewe na mwanao mtakuwa salama.

    Muddy

    ReplyDelete

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.