Habari za Punde

*TWIGA STARS ENDELEENI KUWAFUTA MACHOZI WATANZANIA, ENDELEENI KUWAPA RAHA WATANZANIA

 *SI WAKATI WA KUPONGEZWA NI WAKATI WA VITA KUJIANDAA NA ILIYO MBELE YENU.

*MSINGI PEKEE WA KUISHINDA VITA HIYO NI KUJITUMA NA UTAIFA KWANZA.

TIMU ya Taifa ya Wanawake Tanzania, Twiga Stars, jana imeweza kuwafuta angalau machungu na machozi watanzania kwa kuwatoa kimasomaso baada ya kushinda michezo yote miwili wa ndani na nje kwa kuwafunga Namibia kwa jumla ya mabao 7-2 na kufanikiwa kutinga katika hatua ya pili ya kutafuta tiketi ya wania kufuzu kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake, zinazotarajia kufanyika mwezi Juni mwaka huu.

Pamoja na ushindi huo mnono na wenye kuwafurahisha watanzania wale waliofika uwanjani kuwashangilia na hata wale waliokuwa majumbani wakifuatilia mchezo huo kupitia Luninga zao, basi DADA ZETU, jitahidini kudumisha furaha zao kwa hali na mali kadri muwezavyo.

Na huu si muda wa kuwapongeza dada zetu wala kuwasifia kwa kalamu zetu kupitia karatasi za magazeti yetu na vyombo mbalimbali vya habari kwani kwa kufanya hivyo tutawapotosha hawa Dada zetu na hata wakaona kuwa labda tayari wameshavuka mto wenye Mamba wengi na wakali hivyo wakapunguza spidi na kujiamini.

Badala yake, kupitia kalamu zetu tuwape changamoto mbalimbali wachezaji wtu na walimu kwa umoja, ushorikiano na upendo tu, kwa yale yanayoweza kutuwezesha kuvuka mto ulio mbele yetu na hatimaye kufika pale tunapopahitaji ili tuweze kushangilia matunda kwa uhuru usio na presha.

Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ni wakati wetu sasa kuwapa moyo wanadada hawa waliotutoa kimasomaso ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kwa michango inayoweza kuwawezesha kukidhi mahitaji yao kwa kipindi hiki kigumu kilichombele yao na suluhisho si kugoma kwa wachezaji kama walivyofanya madaktari bali ni uvumilivu wa wachezaji na kujituma kwa moyo huku walitambua kuwa hivi sasa wao ndiyo hasa jicho la nchi linaloangaliwa na kila mtu.

Baada ya ushindi wa jana wa timu hiyo ya Twiga sasa wanatarajia kukutana na timu machachari ya Misri kama si Ethiopia ambao nao walikuwa vitani jana huku timu ya Misri ikiwa na uhakika baada ya kuwachapa Ethiopia mabao 4 katika mchezo wao uliopita.

Hivyo basi timu hizo zote mbili si za kubeza wala kuzarau na hasa Misri kwa hiyo mwalimu wetu wa Twiga, Boniface Mkwasa, ana kazi ya ziada kwa kipindi hiki kifupi na hasa kwa kuwajenga kisaikilijia wachezaji wetu na kuwapa mazoezi ya kuwaweka fiti na ya kuongeza spidi ya mchezo.

Pamoja na kucheza soka safi jana na kuibuka na ushindi, lakini bado pia timu ijiandae zaidi na kuongeza spidi ya mchezo ili kuweza kuwamudu hao 'Misri ama Ethiopia'.

Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, unawapongeza wanadada wa Twiga Stars na wale wote waliofanikisha kwa namna moja ama nyingine kufanikisha ushindi huo. ''SHIME DADA ZETU TWIGA STARS, SILAA BEGANI MSIGEUKE NYUMA''


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.