Habari za Punde

*SHUGHULI ZA MSIBA NA SARE KWA WANAMAMA!

Unapokutana na wanamama kama hawa wakiwa katika sare zao zilizopendeza na za rangi moja waweza fikiri wapo katika shughuli ya furaha, harusi na nyinginezo, lakini kamera ya Sufianimafoto siku za hivi karibuni ilikutana na TASWIRA hii iliyo tofauti ambayo kwa kweli imekuwa ni tofauti na siku za nyuma.
Wanamama hawa wakiwa wamevalia sare zao wakiwa eneo la Makaburi ya Sinza wakitoka kuzika, yaani utazani walijua kuwa msiba huu utatokea na kuandaa sare hizi, cha kushangaza wanaweza kuziandaaje sare hizi kwa kipindi kifupi tu pindi unapotokea msiba? tena sare zenyewe ni za kushonesha si Khanga za kununua tu Kariakoo kama ambavyo imezoeleka.

Pia siku za hivi karibuni niliwahikutana na Gari lile lililomaalum kwa kubebea Maiti likiwa limepambwa vilivyo, lakini mbele ya gari hilo pia kulikuwa na cha kushangaza, kwani lilikuwa likiongozwa na gari la Matarumbeta yaliyokwa yakirindima vilivyo njia nzima.

''Ama kweli Msiba ni Sherehe ya mwisho wa maisha ya Mwanadamu''!!!

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.