Habari za Punde

*AJALI YA BASI LA NEW FORCE LAUA WANNE NA KUJERUHI, IRINGA

Na Francis Godwin, Iringa
SIKU moja tu baada Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christina Ishengoma, kuwatunuku vyeti na kuwapongeza askari 11 akiwemo mkuu wa kikosi cha usalama barabarani (RTO) Kedmund Mnubi na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Claus Mwasyeba, kwa kusimamia kazi nzuri ya kuepusha ajali mbaya mkoa wa Iringa, ajali mbaya imetokea wilayani Mufindi mkoani Iringa na kusababisha Vifo vya abiria wanne ambao walifariki papo hapo na mmoja kufia hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya basi la kampuni ya New Force lenye namba za usajili T666 BCR lililokuwa likisafiri kutoka jijini Dar es Salaam Kwenda Mkoani Mbeya kupinduka.

Mmoja kati ya abiria walionusurika katika ajali hiyo aliyejitambulisha kwa jina la, John Sanga, alisema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha basi kwa mwendo kasi na uzembe mwingi na hata abiria walipojaribu kumkanya alishindwa kusikiliza na kuwapuuza.

Katika ajali hiyo zaidi ya abiria wengine 16 walijeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi huku wengine zaidi ya 20 wakipata michubuko midogo midogo waliotibiwa na kuruhusiwa .

Aidha mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9 alasiri jana wakati basi hilo likielekea mkoani Mbeya na kuwa chanzo ni mwendo kasi na uzembe wa dereva.


Alisema eneo hilo ambalo ajali imetokea ni eneo ambalo linamteremko na kuwa mbali ya basi hilo kupinduka pia magari mengine Mawili likiwemo gari la serikali lenye namba za usajili STK 2340 na IT yamegongana na Lori katika eneo hilo.

Maiti zilizotolewa katika ajali hiyo hadi saa 2.usiku zilikuwa ni nne na hadi mwandishi wa habari hii anatoka eneo la tukio jitihada za kunyanyua basi hilo ili kutazama maiti wengine zilikuwa zikieendelea chini ya usimamazi wa mkuu wa wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu, na mkuu askari wa Kikosi cha usalama barabarani wakiongozwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa Kedmundi Mnubi.

Majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa katika hospital hiyo ya wilaya ya Mufindi ni pamoja na mtoto wa kiume wa mwaka mmoja ambaye mama yake alikufa katika ajali hiyo , Alen Kilima mkazi wa Kyela , Mwanahabari wa radio Kyela Fm Prakseda Mburu (24) ,Maria Mtawa (46) mkazi wa Tukuyu, Lutusyo Kabenjela (45) mkazi wa Kyela, Elizabeth Andwer(27)Dina Mwasongela (14) mwanafunzi wa kidato cha tatu sekondari ya Lutengano Mbeya, Alex Mwaibambe (28) mwanafunzi wa mwaka wa pili injinia katika chuo kikuu cha Dar es Salaaam, Amon Luvanga (30) mkazi wa Mbeya,Yohana Mwasomola(28)

Wengine ni Aggrey Mwangulu (56) mfanyakazi wa TRA Kibaha , Runna Mwampate (36) mkazi wa Kilawani Dar es Salaam , Iman Mwakifwage (32) mkazi wa Mbeya

Mbali ya majeruhi hao kulazwa katika Hospital ya wilaya ya Mufindi baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika Hospital ya wilaya ya Ilembula wilayani Njombe.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Claus Mwasyeba alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa majeruhi Ramadhan Kipangule (28) mkazi wa Tukuyu Mbeya amefariki usiku wa leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya wilaya ya Mufindi.

Alisema kuwa kati ya abiria waliokufa katika ajali hiyo watatu ni wanawake na abiria wawili ni wanaume na mmoja ametambuliwa kwa jina la ramadhan Kipangule (28) mkazi wa Uyole Mbeya .

Hata hivyo alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea kumsaka dereva wa basi hilo Yahaya Abdalla (35) mkazi wa Dar es Salaam na msaidizi wake Nasib Salum ambao baada ya ajali hiyo walikimbia.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista kalalu amewataka wananchi popote pale nchini kujitokeza kutambua miili ya marehemu hao akiwemo mwanamke huyo aliyeacha mtoto wa mwaka mmoja na nusu










No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.