Habari za Punde

*VODACOM FAUNDATION YAKABIDHI MADARASA 3 NA MADAWATI 100 S/MSINGI RUVU DARAJANI

 Ofisa Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba kushoto akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo mkoani pwani, baada ya kuwakabidhi rasmi vyumba vitatu vya madarasa na madawati 100 kwa ajili ya shule hiyo, msaada huo umetolewa na Vodacom Foundation ambapo umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 98.
*********************************************
 KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania jana ilikabidhi vyumba vitatu vya madarasa pamoja na madawati 100 kwa shule ya msingi ya Ruvu Darajani, Chalinze mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya pili ya mradi wa kuiboresha upya shule hiyo unaofadhiliwa na mfuko wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation.

Madarasa hayo pamoja na madawati yamegharimu zaidi ya shilingi Milioni 90 zilizotolewa na Vodacom katika mwaka wa fedha wa 2011/12 kwa ajili ya mradi huo.

Akikabidhi madarasa hayo Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Bi. Mwamvita Makamba amesema sekta ya elimu ni moja ya kipaumbele kikuu cha Vodacom katika kusaidia maendeleo ya wananchi, kuboresha vipato na kupunguza umasikini katika jamii na kuwajengea watoto msingi wa maisha bora ya baadae.

Vodacom mwaka 2010 iliamua kuijenga upya shule hii baada ya kuguswa na uchakavu wa majengo ulioweza kuathiri utoaji wa taaluma huku ikiwa inahudumia mamia ya watoto wa eneo hili la Ruvu Darajani na maeneo jirani ambao wengi wao ni wa kipato cha chini na cha wastani..

"Vodacom iliamua kujenga madarasa mapya na sio kuyakarabati ya zamani ili kutoathiri shughuli za masomo shuleni hapo ambapo wakati wote wa ujenzi masomo yamekuwa yakiendelea katika madarasa ya zamani na wanafunzi huhamia kwa awamu katika vyumba vipya vya madarasa kadri ujenzi unavyokamilika." Alisema Mwamvita

Shule hiyo ya msingi ya Ruvu Darajani ilijengwa mwaka 1964 na haijawahi kufanyiwa ukarabati mkubwa hadi Vodacom kupitia mfuko wake wa Vodacom Foundation ilipoamua kuijenga upya katika mradi wa awamu tatu unaohusisha ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa.

Ili kuhakikisha inatoa kitu kilichokamilika kukidhi mahitaji ya madarasa Vodacom Foundation imekabidhi pia madawati 100 yenye gharama ya shilingi Milioni nane na laki tisa.

"Vodacom ina namna nyingi yakutimiza azma yake ya dhati ya kubadili maisha ya watanzania. Leo tunapoangalia nyuma tunagundua jambo kwamba tumewajengea watoto wetu mazingira bora ya elimu yanayowawezesha kujenga msingi imara wa maisha yao ya baadae".Alisema Mwamvita.

"Vodacom biashara ni sehemu moja ila namna tunavyoshiriki katika juhudi za kubadili maisha ya jamii ni sehemu nyingine muhimu inayotupatia ufahari wa kuwa katika biashara na kwa mantiki hiyo ndio maana Vodacom inawekeza kiasi kikubwa cha fedha kila mwaka kusaidia sekta ya elimu,afya,mazingira na michezo kwa masilahi ya jamii."Aliongeza Mwamvita.
Madarasa ya shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani yaliyojengwa na Vodacom Foundation.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.