Baadhi ya Mawakala wa m-pesa wa Mkoa wa Dares Salaam waliohudhuria katika semina iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala hao kujifunza namna ya kutoa huduma bora za m-pesa kwa wateja wao,Semina hiyo ilifanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Karimjee jijini.
*Mtandao wa Vodacom m-pesa waboreshwa*Kasi yaongezeka.
*Wateja wazidi kufurahia huduma.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imefanya maboresho makubwa katika mfumo unaondesha huduma ya Vodacom m-pesa kwa lengo la kuendana na kasi ya ukuaji na mahitaji ya huduma hiyo katika soko nchini ili kuweza kutoa huduma iliyo bora kwa wateja wake.
Maboresho hayo sasa yanawawezesha wateja wa Vodacom m-pesa kufanya miamala yao kwa ubora na kasi ya hali ya juu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema maboresho hayo makubwa yamefanyika mwezi Disemba mwaka jana ili kuuongeza nguvu na ufanisi mfumo wa mawasiliano unaotumika kutoa huduma za Vodacom m-pesa.
"Tumefanya maboresho kama ilivyodesturi yetu ya kuboresha na kuimarisha huduma zetu mara kwa mara. Tunatambua kwamba wateja wa Vodacom m-pesa walikuwa wanakabiliwa na changamoto za hapa na pale ninayo furaha kubwa kuona kwamba tunaendelea kuiboresha huduma hii"Alisema Bw. Meza
Bw. Meza amesema katika kipindi chote cha mwishoni mwa mwaka huduma ya m-pesa imepatikana kwa kasi na ubora zaidi na hivyo huduma ya m-pesa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kubadili maisha ya wananchi kupitia teknolojia ya simu ya mkononi.
"Wakati wote tunaishi na dhamira yetu ya kutoa huduma bora na kujali mahitaji ya wateja wetu tutaendelea kufanya hivyo mara kwa mara sambamba na kutoa kipaumbele cha kuhakikisha usalama huku tukiongeza pia kasi ya ubunifu na uvumbuzi wa huduma bora". Alisema, Meza.
"Huduma ya Vodacom m-pesa imekuwa kiungo muhimu cha maisha ya wananchi mijini na vijijini imezalisha ajira, imerahisisha maisha na biashara ni kiasi cha kupiga *150#00 kutoka mtandao wa Vodacom na kuanzia hapo kiganja cha mkono kinakusogeza karibu na ndugu jamaa na watoa huduma mbalimbali." Bw.Meza aliongeza.
Huduma ya Vodacom m-pesa imeanzishwa Aprili 2007 na tangu wakati huo ukuaji wake sokoni umekuwa ni wa kasi kufikia wateja milioni tisa kutokana na kutoa urahisi wa malipo na ununuzi wa huduma mbalimbali ikiwemo Maji,Umeme, muda wa maongezi, Dstv, manunuzi ya tiketi za safari za ndege, utumaji na upokeaji wa fedha kwa usalama,uhakika na kuaminika wakati wote ukiwa na mtandao wa wakala zaidi ya elfu ishirini nchi nzima.
No comments:
Post a Comment