Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI SHEREHE ZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KICHINA DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT), zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana jioni
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa  ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana.
  Mmoja kati ya Vijana wanaochukua mafunzo ya Karate katika Kambi ya Klabu ya Tai, iliyopo Mbagala, jijini Dar es Salaam chini ya mwalimu wao Mneke, akionyesha umahiri wake wa kucheza mchezo huo jukwaani wakati wa maadhimisho hayo.
  Vijana wa Tai Club ya Mbagala wakishambulia jukwaa kwa mchezo ya Karate, kwa hakika ilikuwa ni burudani ya pekee iliyotolewa na vijana hawa wa Kibongo.
  Vijana wakimaliza na kuaga jukwaani.
  Baadhi ya wachina na watu waliohudhuria sherehe hizo wakishuhudia matukio yaliyokuwa yakelendelea jukwaani.
 Wanadada wa Kichina wakitoa burudani jukwaani.
 Burudani za wanadaa wa kichina zikiendelea jukwaani, hapa ni wakati waicheza Wakawaka ya kombe la Dunia lililopita.
 Burudani ikiendelea jukwaani.
 Wakimaliza burudani yao na kuaga kwa staili ya kipekee.
 Wanadada wa Kichina wakionyesha umahiri wao wa kupiga vyombo vya ala za muziki.
 Mdada wa Kichina aliyefunika bovu kwa staili zakeza kujikunja, akionysha umahiri wakejukwaani.
 Mdada huyo akiendelea kujikunja nakuonyesha umahiri wake jukwaani.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwa katika pica ya pamoja na baadhi ya wasanii wa kichinana wasiiki waliotoa burudani wakati wa sherehe hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.