Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugay akitekeleza majukumu yake wakati wa Kipindi cha maswali na majibu leo mjini Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wamesimama mara baada ya Naibu Spika wa Bunge Job Ndugay Kuahirisha kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine yaliyojitokeza wakati wa kuahirisha kikao hicho ni hoja ya Mgomo wa madaktari ambayo iliibuliwa na mbunge wa Kigoma mjini, Peter Selukamba, ambaye aliitaka serikali kutoa tamko la hatma ya mgomo huo ambapo Naibu Spika Job Ndugay, aliwataka wabunge kuwa na subira ili Ofisi ya spika ikutane na kamati ya uongozi ya bunge ili kutoa maamuzi hapo kesho kabla ya kuahirisha mkutano huo wa sita.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Longido, Edward Lowasa (kushoto) akijadili jambo na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira, (katikati) na mbunge wa viti maalum CHADEMA Leticia Nyerere leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati) akifurahia jambo na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (kulia) maarufu kwa jina la Sugu (CHADEMA) na mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba (kushoto) nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (Kulia) akizungumza na Zainabu Kawawa mbunge wa viti maalum CCM mara baada ya kumalizika kwa kikao cha saba cha bunge leo mjini Dodoma. Picha zote na Aron Msigwa-MAELEZO
No comments:
Post a Comment