Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWASILI MKOANI RUVUMA KUANZA ZIARA YA SIKU NNE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu,baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mkoani humo kwa ajili ya kuanza ziara yke ya siku nne leo.  Akiwa mkoani Ruvuma, Dkt Bilal atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi katika baadhi ya miradi ya mkoa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma, Delphin Fredrick, ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa vyama vya upinzani waliohudhuria mapokezi ya Makamu wa Rais alipowasili mkoani Ruvuma leo kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku nne. Viongozi wengine wa Upinzani waliokuwapo ni pamoja na Katibu (W) Songea mjini wa Chama cha CUF, Mohmed Makoma, Katibu wa TLP Mkoa Ruvuma, Wellnery Methody Kilowoko na Mwenyekiti wa (W) Songea Mjini TLP, Elias Nchimbi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili wakati wa mapokezi yake kwenya uwanja wa ndege wa mkoani Ruvuma leo Februari 14, 2012 alipowasili kwa ajili ya kuanza zizra yake ya siku nne mkoani hapa.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AAGIZA IFIKAPO APRILI 1 MWAKA HUU WANAFUNZI KUANZA KUPEWA CHAKULA SHULENI
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, akisoma Taarika ya Mkoa kwa Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

Akisoma Taarifa hiyo Mwambungu alisema kuwa tayari amekwishatoa agizo rasmi kwa wakuu wa shule za msingi zote za Mkoa wa Ruvuma, kuanza kutoa huduma ya chakula cha mchana kwa wanafunzi.

Aidha Mwambungu alisema kuwa mbali na huduma ya chakula pia ameagiza shule zoe kuwa na kikundi maalum cha Bendi 'Blass Band' na kuanza ratiba za vipindi vya michezo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wanafunzi kuhudhuria shuleni na kupenda masomo.
 Baadhi ya watoto wa shule za msingi za mkoani Ruvuma wakiwa pembezoni mwa barabara wakati wa mapokezi ya Makamu wa Raid mkoani hapa leo mchana.
Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi za mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.