Na scolastica komba, Kibaha.
Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ndugu ERNEST MANGU wakati akizungumza na mwandishi wa mtandao huu mjini Kbaha leo mchana.
Tukio hilo limetokea tarehe 31/01/2011 majira ya 12:00 mchana huko Kitongoji cha Akupendae Kijiji cha Watoto waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo kuwa ni Pili Miraji Umri Miaka 3, na Zena Miraji mwenye Umri wa Mwaka 1.
Kamanda MANGU amesema chanzo cha tukio hilo ni moto uliokuwa umeachwa jikoni na wazazi wa watoto hao Miraji Rajab Umri Mika 30 ambaye alitoka na mkewe kwenda shamba na kuacha moto huo uliodaka nyasi na kuteketeza watoto na vitu vyote vilivyokuwemo.
Amefafanua kuwa na thamani ya mali zingine zilizoteketea katika nyumba hiyo bado hazijajulikana na miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa ndugu zao kwa mazishi.
Katika tukio lingine, Gari namba T.984 ASB Mitsubishi Fuso likiendeshwa na Ally Juma mkazi wa Moshi akitokea Dar es Salaam kwenda Moshi iligongana uso kwa uso na Gari namba T.850 APG Mitsubishi Fuso iliyokuwa inaendeshwa na George Yohana mkazi wa Hidaru Mkoa wa Kilimanjaro akitokea Kilimanjaro kwenda Dar es Salaam.
Kamanda MANGU amesema Mnamo tarehe 01/02/2012 majira ya saa 8:00 usiku huko katikati ya daraja la mto Wami Wilaya ya Bagamoyo ambapo katika ajali hiyo dereva wa Gari namba T.984 ASB Ally Juma alipata majeraha na kutibiwa kwenye kituo cha Afya Lugoba na kuruhusiwa.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni kufeli break kwa gari lililokuwa likiendeshwa na Ally Juma wakati akishushu mteremkoa wa mto Wami na kwenda kuligonga gari lililokuwa limeshafika katikati ya daraja.
Amefafanua kuwa ajali hiyo ilipelekea adha kwa watumiaji wa barabara hiyo ya Chalinze - Segera kwa barabara hiyo kufungwa na imefunguliwa leo saa 09:45 asubuhi.
No comments:
Post a Comment