Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS KT. BILAL ASISITIZA MAFUNZO KWA WATUMIAJI WA MAJIKO SANIFU DAR ILI KUPUNGUZA UKATAJI WA MITI KUCHOMA MKAA


Na Mwandishi Wetu, Rufiji
SERIKALI imeeleza kuwa iko mbioni kutafuta njia mbadala ya matumizi ya nishati ya majiko sanifu ikwa na lengo la kuhifadi mazingira mikoani ikiwa ni pamoja na kuzia ukataji wa miti ovyo ka lengo la kuchoma mkaa.
 
Hayo yaeelezwa na Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akijibu taarifa ya Mkoa iliyoandaliwa wakati wa mapokezi yake na kusomwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwamtumu Mahiza katika siku ya kwanza ya ziara yake katika Wilaya ya Rufiji.
 
Bilal alisema kuwa pamoja na juhudii kubwa iliyofanywa na wananchi kwa kushirikiana na serikali kwa kuwa na mpango maalum wa kupanda miti zaidi ya milioni moja na nusu na mkoa huo kuvuka lengo hilo kwa kupanda miti zaidi ya milioni 2, lakini bado juhudi hizo hazitakuwa na mafanikio endapo miti itaachwa ikikatwa na kuchomwa mkaa na kuingizwa jijini Dar es Salam.
 
“Kwanza niwapongeze kwa juhudi za kupada miti na kuvuka lengo la serikali la kutaka kila wilaya upanda miti mil. 1.5, lakini juhudi zenu haziwezi kuwa na manufaa zaidi endapo kasi ya kukatwa miti na kuchomwa mkaa inayoingia jijini Dar es Saaam haitadhibitiwa,

Alisema kuwa njia mbadala kwanza ni kurahisisha na kutoa mafunzo kutafuta njia ya kuwafanya watumiaji wa mkaa wa jijini Dar es Salaam, waweze kutumia majiko sanifu na rahisi.
 
Akizungumzia elimu, Dkt. Bilal amepongeza juhudi za ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari sanjali na kuwepo kwa wanafunzi wa kutosha na hakusita kuwapa changamoto ya kudhibiti mimba kwa wanafunzi.
 
“Pamoja na juhudi zote za kujenga na kuwapata wanafunzi wa kutosha tatizo la mimba kwa wanafunzi linapaswa kuzingatiwa,” alisema Makamu wa Rais.
 
Awali akisoma taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa Mwamtumu Mahiza imeeleza mafanikio mbalimbali sanjali na changamoto zinazoukabiri mkoa na kueleza mikakati mbalimbali ya kupambana na changamoto hizo.

“Mkoa wa Pwani pamoja na mafanikio iliyoyapata katika kipindi cha mwaka 2005/2011 katika
 
Nyanja mbalimbli, tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tatizo la ajira kwa vijana ambalo tayari tumeshanza kulipatia ufumbuzi, ilieleza katika sehemu ya taarifa hiyo.
 
“Imeongeza kuwa katika ziara hiyo Makamu huyo pia atafika katika kijiji cha Msoga ambapo atazindua kambi ya maarifa ya vijana wapatao 400 ambayo lengo ni kuhakikisha walengwa wanapata fursa ya kujiajiri.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.