'' SASA YAMEISHA JAMANI EEEH''!, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano rasmi wa kutangaza kuhusu kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Rugemalila Mutahaba (kulia). Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri Dk. Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu. Picha na Anna Nkinda-MAELEZO
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'SUGU' (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (wapili kulia) wakipeana mikono ikiwa ni ishara ya kumaliza mtafaruku baina yao na kuondoa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.
No comments:
Post a Comment