Mmoja kati ya wanamama waliofaidika na mradi wa KfW, akipokea kitambulisho cha kupata huduma za afya kwa niaba ya wenzake 600 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa, wakati wa hafla upi iliyofanyika leo mjini Tanga. Wanaoshuhudia pembeni ya Mkuu wa Mkoa, (kulia) ni Mkurugenzi mkuu wa NHIF, Imanuel Humba na Dr. Sweya ambaye ni meneja wa Mradi kutoka NHIF.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kusaidia kupata huduma bora kwa kina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka 5, katika maeneo ya vijijini.
Naibu Mkurugenzi Mkuu, Hamis Mdee, akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu, kuhusu mradi huo unavyotekelezeka kwa kasi Mkoani Tanga kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi.
Baadhi ya kina mama wajawazito waliowawakilisha wenzao 600 wakati wa kupokea vitambulisho vya huduma za afya wakiwa katika picha ya pamoja na wafadhili wa mradi huo wa (KFW) na NHIF.
No comments:
Post a Comment