Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akizungumza wakati wa Bonanza la waandishi alipoalikwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha hilo maalum linaloendelea katika ufukwe wa Msasani Beach Club, hivi sasa. Sitta amepongeza utaratibu wa waandishi kukutana na kupongezana na kuyataka mashirika na makampuni mengine kujitokeza kudhamini na kuandaa Mabonanza kama ilivyofanya kampuni ya Bia ya TBL, ambapo ameahidi kufanya hivyo katika Wizara yake na kuandaa hafla kama hiyo na waandishi mambo yatakapokamilika. Kulia ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto.
Mchezo wa Soka ukiendelea ufukweni.
Mwandishi wa Sibuka Fm na wengine wakiwa kazini kuhakikisha wananasa matukio yote yaliyokuwa yakiendelea mahala hapo.
Waandishi wakiselebuka na sebene la bendi ya Fm Academia, wakati wa Bonanza hilo.
Waandishi wakisebeneka na sebene la bendi ya Fm Academia, wakati wa Bonanza hilo.
Wanenguaji wa bendi ya Fm Academia, wakishambulia jukwaa kwa fujo na miondoko ya bendi yao.
Wanenguaji wa bendi ya Fm Academia, wakishambulia jukwaa kwa fujo na miondoko ya bendi yao.
Wanamuziki wa bendi ya Fm Academia, wakishambulia jukwaa kwa fujo na miondoko ya bendi yao.
Rapa na mwimbaji wa bendi ya Fm Academia, Totoo Kalala, akighani rap zake kusebenesha waansihi waliokuwa wakisebeneka stejini.
Waandishi wakiselebuka na sebene la bendi ya Fm Academia, wakati wa Bonanza hilo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Muddy kutoka kundi la Fela TMK, akionyesha umahiri wake wakati akitambulishwa jukwaani na kuimba.
Mh. Temba na kundi lake wakishambulia jukwaa.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kikifanyika jukwaani
Waandishi wakiselebuka na sebene la bendi ya Fm Academia, wakati wa Bonanza hilo.
Bibi Cheka na Mh. Temba na kundi lao wakishambulia jukwaa.
Bibi Cheka na Mh. Temba na kundi lao wakishambulia jukwaa.
Bibi Cheka akiendelea kuwapagawisha mashabiki wake jukwaani.
Baada ya Bibi Cheka kushuka Jukwaani, alianguka ghafla na kupoteza fahamu kwa muda, lakini hii imeelezwa na wasanii wenzake kuwa jana alikuwa akiendelea na dozi ya Maralia na kutokana na kwamba tayari alikwishatambulishwa kupanda jukwaani leo na kutambulishwa kwa waandishi wa habari alishindwa kughairisha na kupanda na ndiyo maana aliposhuka alihisi kizunguzungu na kuanguka na kisha kuumia sehemu ya puani. Pichani Bibi Cheka akipatiwa huduma ya kwanza na watu wa msalaba mwekundu baada ya kuanguka.
No comments:
Post a Comment