Habari za Punde

*KAA TAYARI KUPATA KOPI YAKO YA KITABU CHA HASIRA ZA MPANGAJI



MAAJABU YA ULIMWENGU!
*Fahamu mikasa na vituko mbalimbali wanavyofanya baadhi ya wenye nyumba na wapangaji wa hapa Tanzania kwenye nyumba za kupanga, kwa kusoma hadithi yenye vituko vilivyotokea kwenye baadhi ya nyumba: HASIRA ZA MPANGAJI(HM).
*Fahamu pia jitihada mbalimbali wanazofanya wanasayansi wa nchi za magharibi katika kutafiti viumbe hai  nje ya  dunia  (extraterrestrial life). NASA (National Aeronautics and Space Administration) yenye makao makuu yake  Marekani, kwa kupitia projekti yao ya SETI, wanatafiti uwezekano wa kuwa na viumbe wenye akili na utashi kama binadamu wa hapa  duniani. Viumbe vinavyosadikiwa kuishi kwenye sayari  zilizo nje ya mfumo wa jua, kama vile sayari za Kepler-22b, GJ 1214b na Gliese 581d. (Mwanga {300,000km/s} huchukua miaka 20, kusafiri toka duniani hadi sayari ya Gliese 581d).
Utafiti huo hautaleta uhalisia kama utafanyika huku watafiti wakiwa duniani tu. Hivyo, wamejenga maabara yao huko nje ya dunia(International Space Station  au ISS). Ipo kwenye kiwanja kinachoelea  hewani!.  
Wazo la kujenga maabara hiyo ya aina yake liliibuliwa mwaka 1869, baada ya mwandishi wa ki Amerika(Edward Everett Hale) wa  hadithi ya kisayansi iitwayo  “Brick Moon”, kuchapisha hadithi hiyo. Malighafi ya kwanza ya kujengea ISS ilipelekwa kwenye kiwanja hicho novemba 1998.Roketi ya Kirusi ilifanya kazi hiyo.Malighafi  nyingi zaidi ziliongezwa kwa miaka miwili iliyofuata. Mpaka kufikia mwaka 2000, tayari jengo hilo lilifaa kwa watu kuishi ndani yake. Hivyo  kikosi cha kwanza cha wana utafiti kilitua (docking) kwenye jengo hilo  mwezi octoba, 2000.

Mwezi Julai mwaka jana (2011), NASA walikwenda  ISS kwa kutumia usafiri maalumu,ATLANTIS. Mwishoni mwa mwaka jana, Warusi nao wakajitosa huko kwa kutumia SOYUZ.Na hivyo, kuhitimisha ukarabati wa  nyumba hiyo inayoizunguka dunia kila baada ya dakika 90. Yaani, jua huzama na kuchomoza tena, mara 16 kwa siku. ISS ina mabafu mawili na sehemu ya michezo(GYM).  Jengo hilo la kiunajimu, ni kubwa kama nyumba ya vyumba vitano.

Ni changamoto gani wanakutana nazo?. Kwa nini jengo hilo linaelea?. Wanazigunduaje sayari mpya?. Kwa nini  wanahatarisha maisha yao na kuteketeza mabilioni ya fedha ili kuwekeza  kwenye utafiti huo?.Wataalamu mbali mbali  duniani,wanasemaje juu ya utafiti huo?. GYM la nini tena huko nje ya dunia?. Na mengine mengi huenda hujawahi kuyasikia. Usiachwe nyuma, kimbia pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kusoma riwaya ya HASIRA ZA MPANGAJI, uhabarike, uburudike na kujiongezea maarifa ya mtindo huo.
*Waandalie watoto mazingira mazuri ya kuipenda sayansi na teknolojia  kwa kuwazawadia riwaya ya kisayansi: HASIRA ZA MPANGAJI.
*Kwa wapenzi wa kutalii,usikubali kutalii ndani ya dunia tu, ungana  na mwandishi wa HASIRA ZA MPANGAJI usafiri  kwenda nje ya  dunia, uitalii jiografia, sayansi na maisha ya watu wa huko.
 Kwa kanda ya ziwa, HASIRA ZA MPANGAJI inapatikana kwa Tshs 3500/= tu kwa wauza magazeti  na vitabu walio maeneo yafuatayo;
<>MWANZA MJINI(PPF PLAZA,MAKOROBOI,SOKONI,TANESC O,KAMANGA FERRY,0764331568,0755734574)-Pia inapatikana kwenye VICTORIA BOOKSHOP. (BURUDIKA!: BAADA YA MIAKA 1200 TOKA SASA, TEKNOLOJIA YAWEZA KUFIKIA WAPI?,JIBU=HM)
<> KAKOLA (0764361519), KAHAMA (0753574124), MUSOMA-  KAMISA(0755004410), BUKOBA (0713918505,  0754552485), BUNDA(0655282034), TARIME(0765649612), SHINYANGA (0755873500),GEITA(0759419303)  , SENGEREMA(0753982040, 0769359373).
NA HIVI KARIBUNI, ITATUA DAR ES SALAAM.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.