Habari za Punde

*MAN UNITED YASHIKA TENA USUKANI WA LIGI KUU YA ENGLAND

Rooney na Johny Evans wakisherehekea bao

Mshambuliaji wa timy ta Manchester United Wayne Rooney aliifungia timu yake bao muhimu na kuipaisha kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza kwa kuichapa Fulham bao moja bila.

Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza pale Rooney alipopokea pasi safi kutoka kwa Jonny Evans.


Kwa ushindi huo sasa Mashetani wekundi wameipiku Man City kwa alama tatu.

Kufikia sasa timu zote zimecheza mechi 30 kila mmoja.

Manchester City sasa wanakibarua kigumu cha kuziba pengo la alama tatu kwani siku ya jumamosi tarehe 31 wataikaribisha Sunderland.

Vijana hao wa Roberto Mancini itawabidi waombe sana Man U wapoteze mechi yao ya siku ya Jumatatu ijayo tarehe 2 April watakapo watembelea Blackburn.

Hata hivyo mkufunzi wa Fulham Martin Jol amelalama kuwa walinyimwa mkwaju wa penalti.

Hii ni baada da ya Michael Carrick wa Manchester United kuonekana kumuangusha mshambulizi Danny Murphy katika eneo la hatari katika dakika ya 87.

Meneja huyo wa Fulham amenukulikwa akisema kuwa kila mtu aliyeshuhudia mechi hiyo alitarajia wapewe penalti.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.