Mahakama ya nchini Uingereza imemfunga jela mwanafunzi, Liam Stacey, aliyeweka ujumbe wa kibaguzi uliomkejeli mchezaji wa timu ya Bolton Fabrice Muamba, katika mtandao wa Twiteer.
Mcheza soka huyo alizirahi uwanjani baada ya moyo wake kusimama wakati akichezea klabu yake mapema mwezi huu.
Liam Stacey amekiri kuchochea chuki za ubaguzi wa rangi dhidi ya Muamba, ambapo tayari ametupwa jela kutumikia jumla ya siku 56.
Hivi sasa mchezaji huyo Muamba, amepata nafuu japo bado yu po katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Mchuano wa FA kati ya klabu yake ya Bolton na Tottenham ambao ulisimamishwa baada yake kuzirahi unachezwa tena leo usiku.
Habari na picha kwa hisani ya BBC Swahili
No comments:
Post a Comment