Habari za Punde

*TIMU ZINAZOPAMBANA KUTOSHUKA DARAJA VILLA SQUAD NA MORO UNITED KUKIPIGA KESHO

TIMU za Moro United na Villa Squad ambazo ziko kwenye vita ya kujihami na kukwepa kushuka daraja katika Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinashuka dimbani kesho Machi 28, kupambana kusaba Pointi tatu muhimu, ikiwa ni moja kati ya michezo miwili ya Ligi Kuu inayochezwa kesho.
Mechi hiyo namba 153 itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili. Moro United iko nafasi ya 11 ikiwa na pointi 18 wakati Villa Squad iko nafasi ya 14 ikiwa na pointi zake 14.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu. Mwamuzi atakuwa Andrew Shamba akisaidiwa na Samson Kobe na Idd Mikongoti wote wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Arthur Mambeta wa Dar es Salaam wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Emmanuel Chaula kutoka mkoani Rukwa.
Mechi nyingine inayochezwa kesho ni kati ya Ruvu Shooting na itakayokuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar, itakayochezeshwa na mwamuzi Judith Gamba wa Arusha kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Gamba katika mechi hiyo namba 150 atasaidiwa na Saada Tibabimale kutoka Mwanza na Hellen Mduma wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa akiba ni Juma Safisha wa Pwani wakati Kamishna ni Hamis Kissiwa wa Dar es Salaam.
Mechi za Machi 31 mwaka huu ni Coastal Union dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi ya African Lyon na Simba.
 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.