Habari za Punde

*MARIA SOLOMA NA KADO BASS WAPIGWA STOP TWANGA

Baadhi ya wanenguaji wa bendi ya Twanga Pepete, wakiwajibika Jukwaani katika moja ya onyesho lao hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni.
**************************************
Mnenguaji mahiri wa bendi ya African Stars, Maria Soloma na mpiga gitaa la Bass, Kado Bass, wamesimamisha kuitumikia bendi hiyo kwa muda kwa kile kilichoelezwa kuwa na utovu wa nidamu kundini.

Imeelezwa kuwa Maria Soloma, amesimamishwa kutokana na kushawishi makundi ndani ya bendi ikiwa ni pamoja na kushiriki kuhamasisha wanenguaji wenzake akishirikiana na mnenguaji aliyeipa kisogo bendi hiyo, Lilian Internet, ambao kwa pamoja walikuwa wakiwashawishi wanenguaji chipukizi wa bendi hiyo, Mary  Khamis na Cicky Daud ili kutimka katika bendi hiyo.

Na kwa upande wa mpiga bass, Kado imeelezwa kuwa yeye amekuwa ni mtoro kazini ambapo kwa wiki mbili mfululizo amekuwa akifika kazini kwa 'Kubeep' ambapo tayari alishakanywa na uongozi wa ASET bila kujirekebisha mara kadhaa.

Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, kwa njia ya simu Mnenguaji Maria Soloma, alisema kuwa kwa upande wake hatambui kama amesimamishwa kazi kutokana na kuwa hajapewa uthibitisho wowote wala barua inayoeleza juu ya kusimamishwa kazi.

''Mimi wala sijui kama nimesimamishwa kazi ndo kwanza nasikia kutoka kwako, na leo naenda kazini kama kawaida, sasa sijui kama kazi za siku hizi zinautaratibu wa namna hiyo wa kusimamishana kazi bila kupeana taarifa wala barua 'maandishi', kama uongozi wangu umetoa taarifa hiyo mimi haujanitaari hivyo mi wajibu wangu ni kuripoti kazini kama kawaida tu''

Na alipoulizwa kuhusu kuwashawishi wanenguaji wenzake wa kike ili kutimkia kule wanakotimkia wanamuziki wa bendi hiyo, alijibu kuwa yeye hana madaraka yeyote wala hisa na bendi hiyo.

Kwa upande wa kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu, alipopigiwa simu mara tatu na mtandao huu hakuweza kupokea simu ili kuzungumzia utata huu hadi tunapanda hewani.

'' Kwani mimi nimekuwa Mama Sakina, hadi nifanye kazi ya kuwashawishi wanenguaji kuihama Twanga na kujiunga na Mashujaa''? alihoji Maria. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.