Habari za Punde

*MSANII MKALI WA WIMBO WA FACEBOOK KUKAMUA JUKWAA MOJA NA WABONGO KESHO VIWANJA VYA POSTA KIJITONYAMA

 Msanii wa Muziki kutoka nchini Afrika ya Kusini, Cleopas Monyepao (DJ Cloe) (kulia) akizungumza na waandishi wa habari, Dar es salaam leo kuhusu onyesho lake litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama  kesho. Kushoto ni Msanii aliyeongozana naye,  Dumiseni Mkihanya.
Na Mwandishi Wetu

CLEOPAS Monyepao maarufu kama DJ Cleo mkali wa nyimbo ya Facebook kutoka Afrika Kusini kesho anatarajia kutoa burudani katika viwanja vya Posta, Kijitintama jijini Dar es Salaam.

 Dj Cleo ameambatana na wachezaji wake Dumisani Makihanya 'Bleksem' na Dj Soul T ambaye amekuwa akionekana katika video mbalimbali za nyimbo zake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Dj Cleo alisema amefurahishwa sana na ujio wake hapa nchini ikiwa ni mara yake ya  kwanza na hiyo ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili.

Alisema, anaamini katika onesho lake hilo la kesho atajifunza mengi kutoka kwa wasaniiwakali wa hapa nchini na Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kufanya shoo katika jukwaa moja na wanamuziki wa Bongo na kujua utamaduni wa Mtanzania kupitia sanaa.

Aliongeza kuwa anahitaji sana kujifunza utamaduni wa Tanzania kwani nchi hizo zinaushirikiano mkubwa na zinaendana kwa mambo mbalimbali kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na muonekano wa wananchi wake.

Aidha alisema, kwa upande wa burudani atawapa mashabiki burudani nzuri na ambayo wataridhika nayo ingawa mashabiki wake wengi wa Tanzania wanaujua wimbo wake wa Facebook kwa sana kuliko nyingine, lakini yeye ananyimbo nyingi hivyo zitakuwa ni 'Supries' kwao.

"Watu wengi wanaujua wimbo wangu wa Facebook lakini zipo nyimbo nyingi tu ambazo ni nzuri, ambazo zitakuwa ni mpya kwao na ninaamini watazipenda hivyo waje kwa wingi ili waweze kujionea na kusikia," alisema.

Naye kwa upande wake mmoja wa wanamuziki ambao wataimba jukwaa moja na DJ Cleo, Omari Nyembo 'Ommy Dimpoz' alisema, anajisikia faraja kubwa kupanda jukwaa moja na msanii huyo kwani anaimani naye atajifunza mengi kutoka kwa msanii huyo.

Alisema, kupanda jukwaa moja na wasanii wa nje kunawasaidia muziki wao kufahamika Kimataifa zaidi kwani utajulikana ukilinganisha kazi yake hasa mwanamuziki huyo ni ya Udj.

Sambamba na wanamuziki hao pia jukwaa hilo litapambwa na Suma lee, Dully Sykes, Juma Nature, Tip Top Conection, Wanaume Halisi, Chege na Temba, Wanaume TMK na Wakali Dancers

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.