Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya mitaro iliyojengwa na wananchi kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji kuboresha kilimo cha umwagiliaji, Wilayani Rungwe hivi karibuni.
************************************
NA MAGRETH - KINABO – MAELEZO
NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, ametoa changamoto kwa wazalishaji wa chakula nchini kuhakikisha kuwa wanatumia njia sahihi za kilimo cha kitaalamu ili kuweza kuepusha upungufu wa maji na uchafuzi wa vyanzo vyake.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri huyo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya 24 ya wiki ya maji yatakayoanza rasmi Machi 16 hadi 22 mwaka huu.
“Juhudi za pamoja zinahitajika kati ya wazalishaji wa chakula na wasimamizi wa vyanzo vya maji katika kuhakikisha kuwa usimamizi bora wa vyanzo vya maji hususan katika shughuli za kilimo ili nchi yetu iweze kuwa na uhakika wa chakula,” alisema Waziri Lwenge huku akisisitiza kwamba ‘maji ni uhai kwa kila kiumbe bila maji hakuna chakula,’ alisema Waziri Lwenge.
Alisema kauli mbiu ya maadhimisho hayo, ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Iringa kuwa ni ‘Maji na Uhakika wa Chakula,’. Maadhimisho hayo yatafanyika kila mkoa na wilaya nchini.
Aliongeza kuwa mujibu wa takwimu za Shirika la Chakula Duniani(FAO) zinaonyesha kuwa uzalishaji wa chakula duniani umeongezeka kutoka ka kilimo cha umwagiliaji lakini asilimia 15(sawa watu 854milioni) wanakabiliwa na upungufu wa chakula.
Waziri Lwenge alisema kuna umuhimu wa kuongeza kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kukidhi uzalishaji wa chakula kitakachoweza kukidhi watu bilioni 2.7 katika kipindi cha miaka 50 ijayo.
Katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika ambazo ni utoaji wa elimu, semina, maonesho ya bidhaa, uwekaji wa mawe ya msingi katika miradi, mikutano ya hadhara, usafi na michezo, ambapo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi.
No comments:
Post a Comment