Sehmu ya mashabiki wa soka wakiwa katika moja ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.
******************************
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea tena mwsihoni mwa wiki hii kwa michezo mitatu itakayozikutanisha timu sita kwenye viwanja tofauti.
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea tena mwsihoni mwa wiki hii kwa michezo mitatu itakayozikutanisha timu sita kwenye viwanja tofauti.
Timu ya Yanga itakuwa mwenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa kesho (Machi 10 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na Machi 11 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Simba ya Jijini dar es Salaam na Toto Africans ya jijini Mwanza itakayochezwa kwenye uwanja huo huo.
Viingilio katika mechi hizo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 15,000.
Mechi nyingine itakayochezwa Machi 11 mwaka itakuwa kati ya Polisi Dodoma na Kagera Sugar. Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Jumatano ya Machi 14 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili. Simba watakuwa wageni wa Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati Yanga watakuwa wenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment