Mabondia, Selemani Galile (kushoto) na Tomasi Mashali wakitazamana kwa usongo wa kila mmoja kutaka kuchukua mkanda wa ubingwa wa mchezo wa masumbwi wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini TPBO walipokuwa wakitambulisha pambano lao jijini Dar es Salaam jana. Pambano hili linatarajia kufanyika Aprili 9, mwaka huu. Katikati ni Rais wa Oganaizesheni hiyo, Yasin Abdallah Mwaipaya. Picha na Super D
*****************************************************
MABONDIA Selemani Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 mwaka huu kuwania mkanda wa ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa la uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Akizungumza na mtandao huu Dar es Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema kuwa, atahakikisha anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao.
"Mkanda lazima niiuchukue kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.
Naye Mashali, alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wa nani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua zaidi na kuhakikisha anaibuka bingwa na kuziba mdomo wa mpinzani wake.
"Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.
Rais wa TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyemamu ambaye ameandaa pambano hilo hivyo bingwa atakayepatikana ndiyo utakuwa kwake akisubiri mpinzani mwingine.
No comments:
Post a Comment