Kocha wa Dunia, Muumin Mwanjuma akiwa jukwaani na wanenguaji wake wakati akiwa na bendi ya Double M.
*Mashabiki wao nao huoa na kuolewa ‘na wasanii wasiooa na kuolewa’
*Wasanii waliowengi hushuka hushuka kisanii na kupoteza mwelekeo baada ya ndoa
MIMI na wewe mdau wa sanaa mbalimbani za kitanzania, Muziki, Filam na nyinginezo, mchezo wa Soka na mingineyo, tunaweza tusiyaelewe haya kwa umakini badala yake tukabaki na maswali mengi tu yasiyo namajibu, ‘’Mbona msanii Fulani siku hizi hasikiki kazimika, mbona msanii Fulani kapoteza mwelekeo’’, na mengine mengi tu.
Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, umejaribu kufanya utafiti wa kina na kuchonga na baadhi ya wasanii ili kujua ukweli na sababu zinazosababisha wasanii kuteteleka mara baada ya kuoa au kuolewa.
Mafoto imeweza kufuatilia na kuwakumbuka baadhi ya wasanii walioweza kufanya vizuri katika soko la muziki wa dansi, Bongo Flava, Sanaa ya Filam na Soka, na wengine wamepoteza nyota tu ya kupendwa na mashabiki wao tofauti na walivyokuwa kabla ya kuoa au kuolewa.
Na hawa ni baadhi tu ya wasanii walioweza kupatwa na maswahibu hayo:-
MUUMIN MWINJUMA:- ‘Kocha wa Dunia’, huyu yeye kama itakumbukwa aliweza kutamba sana wakati akiwa mwajiliwa katika bendi ya African Revolution ‘Tam tam’ akilipwa mshahara na Mkurugenzi wake Asha Baraka.
Muumin aliweza kutamba na nyota yake kuang’aa sana tangua lipoanza na wimbo wake wa Tunda uliowavutiwa mashabiki wengi wa muziki wa dansi na kuweza kujizolea mashabiki lukuki, ambapo baadaye aliweza kuanzisha bendi yake iliyokwenda kwa jina la Double M, ambayo pia ilifanya vizuri na kuwavutia mashabiki kwa vibao kadhaa na hasa ule wa Kilio cha Yatima.
Baadaye Kocha wa Dunia alitangaza ndoa ya kwanza ambayo haikuweza kudumu na hatimaye kuoa tena na kuzuka mtafaruku uliosababisha kuvunjika tena kwa ndoa hiyo na kasha bendi yake ikaanza kuteteleka na kisha wanamuziki wake mmoja baada ya mwingine wakaanza kutawanyika na akajikuta hana budi zaidi ya kuvunja bendi na kuanza kurekodi kama msanii anayejitegemea.
Baadaye akajaribu kuungana na Choki na kuunda bendi iliyokwenda kwa jina na Double Extra baada ambayo nayo haikuweza kudumu mbali na kurekodi vibao vichache katika Studio.
Lakini juhudi za Kocha hazikuishia hapo kwani aliweza kujitutumua na kuweza kuanzisha bendi nyingine miaka ya hivi karibuni iliyokwenda kwa jina la Bwaga Moyo Sound, ambayo pia haikuweza kukimbizana na ‘speed 100’ ya bendi kongwe na hatimaye nayo ikavunjika.
Baada ya kujaribu kila jinsi na kujaribu kuungana na mastaa wenzake kama Ally Choki na Banza Stone, wakirekodi nyimbo kadhaa kali tu zilizoweza kufanya vizuri, lakini tayari nyota yake ilikwishazimika na hivyo kushindwa kurejea kama awali.
Na sasa Kocha huyo wa Dunia, tayari amekwisharejea kwa mwajiri wake wa zamani na kujiunga na bendi ya Twanga Pepeta, lakini bado haonyesha makeke na kujizolea mashabiki lukuki kama alivyowahi kufanya awali.
************************************************************
************************************************************


Marlow (kushoto) na mkewe Besta
*************************************
JUMA NATURE:- Kama itakumbukwa kwa msanii huyu ilifikia wakati hata akiimba kisichojulikana na kurekodi bado mashabiki walimpenda na kununua kanda zake tu, huku nyota yake ikizidi kung’aa na kujizolea mashabiki lukuki kila kukicha.
Lakini baada tu ya kutangaza ndoa na kuoa, hivi sasa Juma Nature Yule wa enzi za Tina, si huyu wa sasa, kwani ni hivi karibuni tu ndiyo ameanza kuibuka upya kupitia Ukumbi wa Dar Live uliozinduliwa huko maeneo ya Mbagala.

Inspector Haroun na Luteni Karama, wakati walipokuwa kundi moja na Gangwe Mob, hapa wakiwa Studio wakirekodi mawe yao.
********************************************************
IRENE UWOYA NA NDIKUMANA:- Hawa ni wasanii wenye fani tofauti mke ni msanii wa Filam na mume ni mwana Soka, lakini pia baada tu ya ndoa yao iliyokuwa ikiandamwa na vikwazo vya kila aina hatimaye wawili hawa wamekwishaachana, huku Uwoya akizidi kupoteza mwelekeo katika sanaa yake na Ndikumana akizidi kuzimika katika anga ya Soka. Hawa nao pia ndiyo safari imeanza taratibu mara watazimika na hii inatokana na kususwa na mashabiki wao ambao huwapenda wao kama wao mmjoa mmoja.
**************************************************
**************************************************

Kwa upande wake KANUMBA, pia yeye hadi sasa bado anasumbuliwa sana na mama yake mzazi kuhusu ni lini ataoa, lakini yeye humridhisha mama yake kuwa bado ila itakapofika siku ataoa, ila ilanewezekana pia ameona mbali na kuamua kuyatimiza kwanza yale ya baadaye baada ya kutemwa na mashabiki wake na kisha kupoteza umaarufu wa ghafla.
**************************************

Ngasa bado anauwezo ule ule katika soka na bado anafanya yale yale aliyokuwa akiyafanya kabla ya kuoa, lakini mashabiki wake walio wengi wameanza tu kumchukia na kutokuwa na mvuto naye tena kama awali, jambo ambalo ni mawazo potofu.
*************************************************************
SHADRACK NSAJIGWA:- Beki huyu mkongwe wa timu ya Taifa na Yanga, siku hizi awapo mchezoni akishika mpira tu utawasikia mashabiki jukwaani ‘’Babu huyo hana uwezo tena, kaisha amezeeka huyo kocha mtoeee’’, haya yote yasemwayo si ya kweli bali ni yaleyale mawazo potofu tu.
*************************************************************

Nsajigwa alikuwa akishika mpira ama kwenda kumkabili adui jukwaa zima humshangilia, lakini eti baada ya kuoa tu ndiyo yamezuka maneno haya yote, Nsajigwa bado ni Yule Yule kwani hadi sasa tumekuwa tukimuona akifanya mambo yale yale aliyokuwa akifanya awali, japo kweli umri nao unakwenda.
***********************************************
***********************************************
Lakini pia bado kuna baadhi ya wasanii ambao waliliona hili na kuamua kufanya mambo yao kimya kimya na wengine kujiwekea utaratibu wa kutangaza ndoa na kuoa ni mpaka baada ya muda Fulani.


Pia wapo wasanii wengi tu wenye majina makuba na wanaoendele kufanya vizuri katika anga za muziki, lakini bado hawajaoa hadi hii leo na wala hawatabiliki wataoa lini . Kushoto ni AY
************************************************************
************************************************************


‘’Bwana unajua sisi wasanii tunashain, tunafanya vizuri kutokana na mashabiki wetu, na mashabiki wengine wanakuwa wakikupenda wewe kama wewe, lakini unapooa tu wanakuhama na wanahamia kwa msanii asiyeoa.
Sijui ni kwa nini mashabiki wa hapa kwetu wanakuwa hivyo wakati kwa wenzetu msanii anapooa ndo na heshima inaongezeka kwa mashabiki wake na wengine humsapoti kwa kila namna na chati yake huzidi kupanda kwetu ni tofauti, yaani ukioa au kuolewa tu basi na mashabiki nao wanaoa na kuolewa na wasanii wasioa na kuolewa, wanahamisha ushabiki’’. Alisema H-Baba
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura A.K.A Lady Jay Dee, akiwa na mumewe Gadna G Habash, siku walipokuwa wakifunga ndoa.
Hawa wawili ni Mtangazaji na Mwanamuziki bado wanavuma japo si sawa na walivyokuwa siku za nyuma, na wanasongesha maisha bora lakini imetokana na kujipanga kwao kwa kujiandaa na kukabiliana na mabadiliko ya mashabiki wao baada ya kuoana, tumeshuhudia Jumba la kifahari la mwanadada huyu likionyeshwa na hizi ni juhudi na akili za kufikiria maisha zaidi kuliko kujirusha. Hongereni Wanandoa.
***********************************************

***********************************************
No comments:
Post a Comment