Habari za Punde

*WANAUME WA ZIMBABWE WAKATAA 'LIFTI' ZA WANAWAKE KUOGOPA KUBAKWA

 *Mbegu za kiume zawa dili, Wanawake huwashikia mitutu wanaume
*Wanaume wamekuwa wakibakwa na kuvunwa mbegu za kiume


KUTOKA HARARE, ZimbabweWANAUME wengi wamezidi kuwagopa wanawake na kukataa lifti pindi magari ya wanawake yanaposimama kwa lengo la kuwapa msaada wa usafiri, kutokana na matukio mengi makubwa yanayoendelea kutokea nchini humo ya wanawake kuwabaka wanaume na kuwavuna mbegu za kiume kwa ajili ya kufanyia mambo ya kishirikina.

Imetokea siku za hivi karibuni ambapo Mwanadada mmoja aliyejulikana kwa jina Susan Dhliwayo (19), mkazi wa jijini Harare kubainisha haya kwa kusema kuwa jiji hilo kwa sasa limebadilika baada ya kutaka kutoa msaada wa usafiri wanaume na kugoma huku wakisema kuwa wanaogopa kubakwa huku akiwanukuu wanaume hao wakisema.

''Hatuwezi kupanda hilo gari lako, wanawake wa siku hizi hamuaminiki''

''Siku hizi wanaume wa Harare wanawaogopa sana wanawake tofauti na siku za nyuma'',alisema

Susan kwa mujibu wa takwimu na taarifa za nchini humo, wanaume hubakwa kwa kuonyeshwa mtutu wa bunduki au kuwekewa kisu shingoni, wakilazimishwa kufanya tendo la ndoa wanawake hao wabakaji, ambao huvuna kwa kukinga mbegu zao za kiume katika mifuko ya Plastiki.

Akitoa ushuhuda mmoja kati ya wanaume waliowahi kufanyiwa kitendo hicho cha kubakwa,  alisema kuwa alikamatwa na wanawake ambao walimpeleka kwenye nyumba iliyokuwa na Nyoka mkubwa, na kumwambi kuwa iwapo atakataa kuwaingilia kimwili 'yaani mkufanya nao mapenzi',  basi watamwacha katika chumba hicho ili apambane na joka hilo.

Aidha Mwanaume huyo aliendelea kusema kuwa, wanawake hao hufanya kazi ya kumuhamasisha mwanume ili awe tayari kuwaingilia kimwili, na wakati mwingine hufaya bila hata kutumia kinga.

Aliendelea kueleza kuwa baada tu ya kumaliza haja zao, wanawake hao kumchukua mwanaume huyo na kwenda kumtelekeza tu barabarani bila hata ya msaada wowote.

Mwanaume mwingine ambaye pia aliwahi kutekwa na wanawake hao, alisema kuwa tukio hilo lilitokea baada ya yeye kupewa msaada wa usafiri 'Lifti', na kundi la wanawake watatu mjini Harare.


''Mmoja wa wanawake hao alinirushia maji usoni, baadaye wakanidunga sindano' alisema mwanaume huyo.

Alisema kuwa baada ya kudungwa sindano walisimamisha gari kando ya barabara na kumuamuru afanye naao mapenzi 'Ngono' kwa kutumia Kondom ambapo baada tu ya kumaliza tendo hilo walimuacha mwituni akiwa uchi wa mnyama na kutimka zao.

''Kwa bahati nzuri watu waliokuwa karibu na maeneo hayo wakikata nyasi wanisaidia kuwaita Polisi, walionipeleka hospitali kupatiwa matibabu, kutokana na ile dawa niliyodungwa kwani ilikuwa bado inanguvu huku ikinifanya kuwa bado na hamu ya kuendelea kufanya mapenzi
isiyopungua. alisema mwanaume huyo

Katika mfululizo wa matukio hayo nchini humo, mnamo Novemba mwaka jana, wasichana watatu wakiwa na mpenzi wao wa kiume, walifikishwa katika Mahakama ya Harare kwa tuhuma ya kubaka wanaume na kuvuna mbegu zao za kiume.

wasichana hao walikamatwa baada ya kupata ajali wakati wakikimbia baada ya kufanya tukio lao la kubaka na Polisi walipofika eneo la ajali na kupekuwa ndani ya gari la wasichana hao, walikuta Kondom 31 zilizotumika zikiwa kwenye Buti.

Lakini wasichana hao walikana mashitaka hayo na kusema kuwa wao ni Makahaba na walikuwa na walikuwa na shughuli nyingi zilizowafanya kushindwa kuzitupa Kondomu hizo zilizotumika.

Kwa muibu wa Mashitaka ya Mahakama hiyo, wasichana hao wanakabiriwa na mashitaka 17, yakiwemo ya ubakaji na mashambulizi japo wao walijitetea kuwa shughuli yai ni umalaya.

Aidha imeelezwa kuwa pia watoto wa mitaani wa kiume wamekuwa wakichukuliwa na wanawake katika mitaa usiku na kupelekwa katika mahoteli makubwa na kufanya nao mapenzi na kisha huambia wakabidhi Kondomu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.