Magari aina ya Fuso, yakiwa yamesheheni magunia ya mkaa yakitokea barabara ya Kiwangwa kuelekea Bagamoyo mjini na kisha jijini Dar kwa ajili ya kuuza.
Pamoja na kelele zote zinazopigwa na Serikali kwa wananchi kuhusu ukataji hovyo wa misitu kwa ajili ya kuchoma mkaa ili kuzuia uharibifu wa mazingira, lakini bado wananchi wamekuwa wakiendelea na ukataji wa misitu na uchomaji wa mkaa tena kwa wingi jambo ambalo husababisha uharibifu wa mazingira na kukua kwa amabadiliko ya Tabianchi, kwa hali hii sasa ni nani wa kulaumiwa ili kupunguza uharibifu huu, alaumiwe Mchomaji wa mkaa, anayekata misitu, alaumiwe mfanyabishara anayenunua mkaa huo na kwenda kuuza kwa watumiaji au alaumiwe mtumiaji???, Akidhibitiwa mmoja kati ya hawa angalau tatizo hili linaweza kupungua kwa kiasi fulani.
Jamaa huyu naye kama alivyonaswa katika Barabara hiyo hiyo, akifunga Kuni katika Pikipiki yake akitokea Kiwangwa kuelekea Bagamoyo, hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment