Habari za Punde

*UWAZI NA USHIRIKISHWAJI WA WAFANYAKAZI NI SILAHA YA MAHUSIANO BORA KAZINI

NA MAGRETH   KINABO – MAELEZO

*Uwazi, na ushirikishawaji hupunguza migogoro kazini.

 IMEELEZWA kuwa  uendeshaji wa taasisi kwa uwazi , usikivu wa  viongozi na  uongozi wa pamoja kati ya menejimenti na wafanyakazi katika  kupanga mipango na  kuweka maamuzi mbalimbali ndio nguzo kuu ya uboreshaji wa mahusiano  mahali  pa kazi.

Hayo yalisemwa leo (jana) na Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Anga Tanzania(TCAA) ,Fadhili Manongi wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kutia saini mkataba  mpya  wa Ushirikishaji wa Wafanyakazi na Baraza la Wafanyakazi na  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya(TUGHE) na mamlaka hiyo.

Utiaji saini wa mkataba huo wa miaka mitatu ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya  mamlaka hiyo ambapo viongozi mbalimbali wa pande zote hizo walisaini.  Miongoni mwa viongozi waliotia saini makataba huo ni Manongi, Katibu Mkuu Msaidizi Taifa(TUGHE),  John Sanjo na  Katibu  wa TUGHE Mkoa wa Dares Salaam, Gaudensi Kadyanga. 

“Hakuna matatizo katika tawi letu pale inapotoekea tofauti tunakaa chini tunaelezana.hivyo ni vizuri kwa viongozi mahali pa kazi kuwa wasikivu wa mambo mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi kwa kuwa wao ndio wanaojua mambo mengi kuliko sisi tunavyojua.

“Hivyo  kuna umuhimu wa  kuwashirikisha wafanyakazi  mambo mbalimbali na bajeti   kwa kuwa wanaweza kuishauri menejimenti  ili kuweza kupunguza athari  zitakazoweza kujitokeza,” alisema Manongi.

Aliongeza kuwa pia yanapotoea mafanikio mahali pa kazi ni vizuri kutoa maotisha kwa wafanyakazi ili kupunguza migogoro na uchangia kuongeza ari ya kufanya kazi.
  
Naye Mwenyekiti wa   Tawi la TUGHE la mamlaka hiyo, ambaye pia alitia saini mkataba huo, Eugene Lwala alisema mamlaka hiyo imefanikiwa  kuboresha mahusiano hayo kutokana   kuwa viongozi wa pande hizo zote mbili kuheshimu mipaka yao ya kazi , kuvumiliana na vikao vya mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.