Mabondia Mada Maugo (kushoto) na Francis Cheka, wakipima uzito kwa ajili ya pambano lao la ubingwa IBF Afrika, linalotarajia kufanyika kesho kwenye Ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam.
*********************************
*********************************
KUNDI la Muziki wa Kizazi kipya linaloundwa na wasanii wakali wawili, Inspector Haroun na Luten Karama, linatarajia kufanya makamuzi katika pambano la ngumi la mahasimu wawili, Francis Cheka na Mada Maugo, linalotarajia kufanyika kesho kwenye Ukumbi wa PTA.
Kundi hilo lililowahi kufanya vizuri siku za nyuma katika jukwaa na muziki huo na kukimbiza vilivyo, baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu sasa limejipanga kuanza mashambulizi upya na kukimbizana na wakali wanaotamba kwa sasa katika fani hiyo.
Pambano hilo la mabondia wenye upinzania mkubwa, Cheka na Mada litakuwa ni raundi 12, katika uzito wa Kati.
Mshindi katika pambano hilo kali atanyakua Mkanda na Gari aina ya Mark ii Toyota Grande lenye thamani ya
shilingi milioni 8.
Mabondia hao walioisha chapana mara kadhaa na mmoja akiibuka mshindi kwa Pointi chache wamekuwa na upinzani mkubwa na kuvuta hisia za mashabiki wengi wa mchezo huo wa ngumi, huku kila mmoja akitamba kumchapa mwenzake kwa K/O na kuondoka na gari hilo.
Kwa upande wake
Maugo alisema kuwa kwa maandalizi aliyoyafanya ana uhakika wa kushinda pambano
hilo, na kuwaomba waamuzi watende haki katika mchezo huo katika maamuzi yao ili mshindi
apatikane kihalali.
“muda wa kuongea
umekwisha hivyo vimebaki vitendo, nipo tayari kwa pambano lakini kubwa ninawaomba waamuzi watende haki na mshindi apatikane
kihalali,”alisema Mada
Kwa upande wake Cheka, alisema
Maugo si lolote kwake na atamfundisha kazi mapema tu na amejiandaa ipasavyo na
mpambano huo ambao anaamini ataibuka na ushindi.
Naye mwandaaji wa
pambano hilo Lucas Ruta kupitia kampuni ya Kitwe General Traders, alisema kwamba
maandalizi yamekamilika ambapo kutakuwa na ulinzi wa uhakika kwa mashabiki na mali zao kwa watakaojitokeza kushuhudia.
Alisema pambano
hilo litatanguliwa na mengine nane ya utangulizi hivyo amewaomba mashabiki wa
mchezo huo kujitokeza kwa wingi na mapema na kuwashudia wasanii wa kundi la Gangwe Mob ambalo litatoa
burudani.
No comments:
Post a Comment