Baadhi ya wachezaji wa timu ya Al-Ahly ya Sudan, wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,leo kwa ajili ya kukipiga na Simba, siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na Stori kwa hisani ya Mama Pipiro blog.
****************************
TIMU ya Al-Ahly ya nchini Sudan, imewasili nchini leo ikiwa na msafara wa watu 30 wakiwamo wachezaji
na viongozi wa timu hiyo kwa
ajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Simba, ambapo mgeni rasmi katika mchezo huo ametajwa kuwa anatarajiwa kuwa
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Timu hizo zitakwaana Aprili 29 katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa 16 bora ya kombe la Shirikisho
Barani Afrika (CAF).
Akizungumza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
Kimataifa wa JK Nyerere, Kocha mkuu wa timu hiyo, Kouk Mohammed, alisema kuwa mchezo huo uantarajiwa kuwa na
ushindani mkubwa kutokana na kuwaona Simba katika baadhi ya michezo yao huku akilinganisha na timu yake.
Aidha alisema anaifahamu Simba kama moja ya timu mahiri
Barani Afrika sambamba na kuwa na uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa hali
ambayo itawafanya wawe makini zaidi watakaposhuka dimbani.
Hata hivyo kocha huyo raia wa Tunisia alisema kwamba
huenda wakaathiriwa na hali ya hewa ya Tanzania kutokana na kuwa tofauti na
Sudan ingawa alisema watajitahidi kukabiliana nayo.
Kikosi cha Al
Ahly kinaundwa na wachezaji watano wa kimataifa wakiwemo wawili kutoka Nigeria ,
mmoja kutoka Mali huku wachezaji wawili wakiichezea timu
ya Taifa ya Sudan .
Al Ahly wanakutana na Simba baada ya kuitoa Ferroviario
ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 3-0, huku Simba iliitoa Es Setif ya Algeria huku
Simba ikibebwa na bao la ugenini baada ya nyumbani kushinda 2-0 kabla ya kwenda
kufungwa 3-1.
Katika hatua nyingine tiketi kwa ajili ya kushuhudia
mpambano huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo katika vituo tofauti jijini Dar es
salaam huku waamuzi wa mchezo huo kutoka Swaziland, Nhleko Simanga Pritchard,
Mbingo Petros Mzikayifani,Sibandze Thulani, Fakudze Mbongiseni Elliot na
Kamishna wa Kayijuga Gaspard wa Rwanda wanatarajiwa kuwasili leo.
Katika kujiandaa na mchezo huo, Simba imepiga kambi
eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam ambapo kocha mkuu wa Simba Mserbia
Milovan Cirkovic amejigamba kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira
mazuri kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili zijazo katika jiji la
Shandy , Sudan .
No comments:
Post a Comment